Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe. Deusdedith J. Katwale amewataka ma Afisa Ugani katika Halmashauri ya Chato kwenda kusimamia na kuwaelekeza wakulima kilimo bora na chenye tija ili waondokane na kilimo cha mazoea.
Mhe. Katwale ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa akikabidhi pikipiki 44katika viwanja vya Makau Makuu ya Halmashauri zilizotolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo na Mifugo ikiwa lengo ni kuboresha utendaji kazi kwa ma Afisa Ugani katika shughuli zao za kila siku. .
Aidha Mhe. Katwale ametoa maagizo 4 ambayo amewataka kila Afisa Ugani aende akayaishi na kuyatenda katika eneo lake la kazi;
Mosi amewataka kuwa wabunifu katika kazi zao ili hata watakapo hamisha au kukoma utumishi wa umma basi wawe wameacha alama.
Pili amewataka kwenda kuwa mfano na kutatua changamoto za wakulima kwa kuhakikisha kila mmoja anakuwa na shamba darasa katika eneo lake ili hata wakulime wengine waweze kujifunza kutoka kwao.
Tatu amewataka kila mmoja kuhakiisha anaanzisha mashamba ya mfano katika taasisi za umma zilizopo katika maeneo yake mfano katika shule na vituo vya kutolea huduma za afya.
Mwisho amewataka kila mmoja aende akatutumie chombo alichopewa kwa kufuata taratibu zote zilizotolewa na Serikali juu ya matumizi sahihi pamoja na utunzaji wake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chato Mhe. Christian Manunga amewataka ma Afisa Ugani kutumia pikipiki hizo walizopewa kama chachu katika kuboresha huduma za ugani katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuonyesha tija ili imani aliyowapa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suhulu Hassan isiwe ni kazi bure hivyo "nendeni mkajipambanue kwa kufanya kazi kwa ubora na uaminifu mkubwa" amesema Manunga.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hamashauri Chato Ndg. Philipo Shoni amemhakikishia Mhe. Mkuu wa wilaya ya Chato kuwa maelekezo yote aliyoyatoa atakwenda kuyasimamia ikiwa ni pamoja na kuhakikisha pikipiki hizo zinakwenda kutumika kama ilivyokusudiwa na Serikali.
Katika hatua ingine ma Afisa Ugani wamepata fursa ya kupata Eimu ya Awali juu ya vyombo vya Moto(pikipiki) kutoka kwa OCS Chato ambaye amewaasa kuhakikisha wanakwenda kujifunza katika vyuo vinavyotambulika na baadae kupata lesseni ili wawe salama wanapotumia vyombo hivyo hata ikitokea wamepata ajali au kusababisha kwani lesseni itakuwa ni kinga kwako kutopata madhara makubwa tofauti na ukiwa huna lesseni ya udereva.
Katika hatua ingine OCS Chato amewataka kuhakikisha wanatumia nguo maaluma wanapoendesha pikipiki hizo hasa kuvaa kofia ngumu kichwani, suruali, viatu, soksi za mikononi pamoja na koti zito ili kulinda afya zao.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.