Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, imefanya kikao na viongozi wa vyama vya Siasa kutoka majimbo ya Chato Kusini na Chato Kaskazini, chenye lengo la kutoa elimu ya maadili ya vyama vya Siasa ili wakazingatie na kufuata Sheria, Kanuni na taratibu za vyama vya Siasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani utakaofanyika 29, Oktoba 2025.
Kikao hicho kimeongozwa na Bi. Dinna Mcharo aliyeambatana na Ndg. Nangalya Ninalwo wote ni Maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa pamoja na Ndg. Herman P. Matemu Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Geita,a Septemba 19, 2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato ambapo amewataka viongozi hao wa vyama kufanya mikutano ya kampeni kwa amani na utulivu badala ya lugha za matusi na kejeli, kuepuka kuchochea ukabila, udini na ukanda pamoja na kuepuka kuwa chanzo cha vurugu badala ya kutangaza Sera Mgombea anatukana, hivyo ametaja adhabu zilizopo ni pamoja na kufungiwa kufanya kampeni.
Bi. Dinna amewaasa viongozi hao wakati wa harakati za uchaguzi wakazingatie kuwa wanawajibu wa kunadi Sera za Chama lakini si ruhusa kunadi Sera zinazokinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, si ruhusa kutoa au kupokea hongo na kuunda kikosi binafsi cha ulinzi,ni ruhusa kupeperusha Bendera ya Chama kwa kufuata utaratibu kama vile eneo wanalofanyia kampeni na maeneo yaliyoruhusiwa lakini sio yaliyokatazwa kama vile Shuleni, Hospitali na maeneo mengine waliyoelekezwa huku akiwasisitiza kutunza amani na utulivu wa nchi kwa kufanya Siasa safi.
Naye Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Geita Ndg. Herman P.Materu amewashauri viongozi hao wa vyama vya Siasa ambao ni wenyeviti na makatibu kuhakikisha wanafanya kampeni za kuhamasisha amani na utulivu kwani amani tuliyo nayo ni wajibu wetu kuilinda, huku akiwasisitiza kuendelea kusoma maelekezo yote waliyopewa na viongozi ili uchaguzi ukafanyike kwa kufuata kanuni taratibu na Sheria.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imekiri kuendelea kutoa semina elekezi zinazowasaidia kuwajengea uwezo viongozi wa vyama vya Siasa lengo likiwa ni kuhakikisha kampeni zinafanyika kistaarabu
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.