Mhe. Christian Manunga ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita ametoa kauli hiyo alipokuwa akikabidhi pikipiki tatu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ajili ya Maafisa Watendaji wa Kata.
Aisha Mhe. Manunga amempongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo anaiongoza Serikali ikiwa ni kwa kusema na kutenda na hili linajidhiilisha katika namna ambavyo Serikali imekuwa na inaendelea kutekeleza Miradi mbalimbali ndani ya wilaya yetu lakini pia katika mkoa na Taifa kwa ujumla.
Ndugu zangu watumishi nimatumaini yetu utendaji kazi sasa katika maeneo yenu utakwenda kuimarika na kuwa chanya hasa katika kusimamia Miradi ya Maendeleo, ukusanyaji wa mapato lakini pia mahusiano na wananchi kupitia pikipiki hizi nayo yataimarika kwani kuanzia sasa mtakuwa na uwezo wa kuwasikiliza wananchi na kutatua kero zao kwa wakati.
Katika ugawaji wa pikipiki awamu hii ya pili, Kata za Bwongera, Nyarutembo na Buziko ndizo zilizopokea na hivyo kufikisha Chato kuwa na pikipiki 10 ambapo kama Halmashauri bado Watendaji 13 hawapokea, ni imani yetu siku chache zijazo wote watakuwa wamepata pikipiki.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Ndg. Elon Mango amewaasa kila mtumishi aliyebahatika kupokea vifaa vya usafiri ahakikishe anazingatia kanuni na taratibu za uendeshaji wa chombo cha moto barabarani ikiwa ni pamoja na kuwa na lesseni
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.