Shirika la Plan international kwa kushirikiana na SEDIT leo limetoa msaada wa Baiskeli 29 kwa walimu wa kujitolea wa vikundi vya ujasiriamali katika ngazi ya jamii kutoka katika kata 7 ambazo Chato, Muganza, Bwongera, Kigongo, Nyamirembe, Bwina na Bukome.
Akikabidhi Baiskeli hizo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chato, Katibu Tawala Wilaya ya Chato ndugu Elias Makory amewataka walimu hao kuzitumia vizuri baiskeli hizo ili ziweze kutimiza malengo yaliyokusudiwa.
"Mmepewa baiskeli hizi, nendeni mkazitumie vizuri, mkafanyie kazi yale ambayo yamelengwa yatimie, lakini najua pia Basikeli hizi pia zitawasaidia ninyi katika kazi zenu binafsi hivyo mnalo jukumu la kuzitumia vizuri" Alisema Katibu Tawala.
Mwenyekiti wa Halmashauri Christian Manunga amesema Baiskeli hizo zikatumike kuhamasisha na kuibua vikundi mbalimbali vya ujasiriamali pamoja na kuhamasisha lishe bora katika shule za msingi na Sekondari ambalo ni moja ya jukumu la walimu hao wa vikundi.
Mratibu wa Mradi wa Kuzuia Ajira Hatarishi kwa Watoto kutoka Shirika la Plan International Wilayani Chato ndugu Leonard Samamba amesema wameamua kugawa Baiskeli hizo kwa walimu wa vikundi hivyo kutokana na kutambua mchango wa walimu wa vikundi hivyo kutokana na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wakati wa utekeleaji wa majukumu yao.
"Sisi tumewekeza kwao, walimu hawa wanatoa elimu kwa vikundi tofauti tofauti, wanavifundisha na tumeona matokeo, hivyo baada ya kuona wanahangaika kufikia vikundi tumeamua kuwagawia Baiskeli hizi ili zikatatue changamoto mbalimbali kwenye ngazi ya jamii.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.