Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amezindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato iliyoundwa baada ya kuunganishwa kwa Mapori ya Akiba ya Burigi, Biharamulo na Kimisi yaliyopo katika Wilaya za Biharamulo, Ngara, Karagwe na Muleba Mkoani Kagera na Chato Mkoani Geita.
Sherehe za uzinduzi wa hifadhi hiyo zimefanyika katika kijiji cha Mkolani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri na Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali hapa nchini, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Viongozi wa Dini, Viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii
Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Mabalozi na wawekezaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kujitokeza kuwekeza katika maeneo ya hifadhi ambayo kwa sasa yana fursa nyingi na pia ametoa wito kwa Watanzania kuhakikisha wananufaika na kuinuka kwa utalii hapa nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangallah amesema kuanzishwa kwa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato kunafanya idadi ya Hifadhi za Taifa kuongezeka kutoka 16 hadi 19 na kwamba wizara hiyo inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha huduma kwa watalii ikiwemo kujenga hoteli 3 za nyota 3 katika maeneo ya hifadhi, hosteli, kujenga gati za maboti ya watalii, barabara na viwanja vya michezo katika hifadhi
Hifadhi hiyo inakuwa ni ya 3 kwa ukubwa hapa nchini ikiwa na jumla ya kilometa za mraba 4,702, ikitanguliwa na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (kilometa za mraba 20,300) na Serengeti (kilometa za mraba 14,763)..
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.