Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni ameahidi kujenga madarasa 7 katika kijiji cha Nyabilezi mahali ambapo kumejengwa uwanja wa ndege wa Chato ulipo kata ya Bukome.
Ahadi hiyo ameitoa leo tarehe 13 Julai 2019 wakati Rais Museveni akiondoka uwanja wa ndege Chato kuelekea nchini Uganda baada ya kumaliza ziara ya siku moja aambapo alifanya mazungumzo binafsi na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Kwa upande wake Rais Magufuli amemshukuru Rais Museveni kwa kuamua kujenga madarasa hayo kijiji hapo na amemwagiza Waziri wa nishati kuhakikisha madarasa hayo yatakapokamilika yanakuwa na umeme.
Mapema akiwahutubia mamia ya wananchi waliokusanyika kumpkea Rais Museveni amesema Tanzania na Uganda zina historia ndefu, na amesema ukiachilia mbali historia ya hizi nchi mbili Tanzania na Uganda kwa sasa kuna bomba la mafuta kutoka Ohima nchini Uganda ambalo linafika Tanga pia ni sababu nyingine ya kuendelea kudumisha umoja baina ya nchi hizi.
Kwa Upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemshukuru Rais Museven kwa kuendelea kudumisha umoja na Tanzania ambapo amemshukuru kwa mambo mengi ambayo ameisaidia Tanzania ikiwemo misaada wakati wa Tetemeko la Bukoba na hivyo kusema ujio wa Rais Museveni ni heshima kubwa kwa Tanzania.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.