Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwa Hospitali Rufaa ya Kanda – Chato itajengwa kama ilivyokusudiwa tangu hapo awali.
Rais Samia ameyasema hayo leo wakati alipotembelea hospitalini hapo akiwa katika ziara ya Siku moja ya kutembelea wilaya ya Chato.“Hospitali hii mpaka sasa majengo matano yapo tayari Niwahakikishie tutaijenga kama ilivyokusudiwa, wataalamu wakutosha wamesha letwa na tutaendelea kuwaleta wengine” Amesema Rais Samia
Aidha Rais Samia amewataka Wananchi wote kujitokeza kwa wingi kujiunga na Bima ya Afya kwa wote pindi itakapoanza kufanya kazi ili kupata Huduma bora za afya katika Hospitali mbalimbali nchini lakini pia kusaidia kunufanisha maendeleo ya sekta ya afya.
Niwaombe sana tutakapo kuja na mfumo wa Bima ya Afya kwa wote, wote tukanunue bima ni kupitia bima hizo tunaweza tukaboresha zaidi huduma hizi za afya” Amesema Rais Samia
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.