Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Ndg. Mohamed Gombati jioni ya leo Agosti 7, 2025 ametembelea katika viwanja vya maonesho ya nane nane Nyamhongolo, Wilayani Ilemela Jijini Mwanza yakihusisha Mikoa ya kanda ya ziwa Magharibi ambapo amekiri kufurahishwa na bidhaa pamoja na huduma zinazopatikana katika mabanda ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato huku akiwaalika wananchi kufika ili waweze kujifunza mbinu bora na za kisasa katika sekta ya Kilimo, ufugaji, biashara na uvuvi kutoka kwa timu ya wataalamu waliobobea.
Hayo ameyasema alipokuwa akitembelea mashamba darasa ya kilimo cha mbogamboga, malisho ya mifugo, ufugaji bora na uuzaji wa ndege mbalimbali kama vile kuku ,njiwa mabata, kanga pia mbwa wenye mafunzo, na bidhaa kama asali, mafuta ya alizeti, samaki wa kukaangwa na kubanikwa bila kusahau watalamu bobezi kutoka idara ya kilimo, mifugo na uvuvi wakitoa elimu hiyo kwa wananchi.
Gombati amesema kuwa maonesho ya mwaka huu yamelenga zaidi faida kubwa kwa jamii kutokana na kila Sekta kuleta shamba darasa lakini pia wataalamu wa kutosha kwa ajili ya kutoa elimu hususani uvuvi kwa kutumia mabwawa, kilimo lishe katika eneo dogo lakini unavuna mazao mengi pamoja na unenepeshaji wa mifugo.
Kauli mbiu; “Chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi 2025”
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.