Baadhi ya wajasiriamali wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kuuziwa vitambulisho eneo la Matabe kata ya Bwanga
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akiwa na mjasiriamali mdogo wa Matabe mara baada ya kupatiwa kitambulisho chake
Baadhi wa wananchi wa Matabe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa (hayuko pichani)
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameongoza zoezi la uuzaji wa Vitambulisho vya wajasiriamali kwa wachimbaji wadogo waliopo Matabe kata ya Bwanga na kijiji cha Musasa kata ya Makurugusi.
Katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa ametoa muda wa siku 4 kwa wachimbaji hao waliopo katika maeneo ya Matabe na Musasa kuhakikisha wanakuwa na vitambulisho hivyo ili Serikali iweze kuwatambua kwa shughuli wanazofanya.
Akiwa katika eneo la Machimbo la Matabe, Mhandisi Gabriel ameliagiza jeshi la Polisi kuwakamata na kuwaweka ndani viongozi wa chama cha ushirika cha wachimbaji wadogo cha Iponyabuhabi kwa tuhuma za kuchangisha fedha kwa wananchi wa maeneo hayo ili waweze kupata leseni ya uchimbaji lakini baada ya leseni kuwa iimekamilika viongozi hao walijimilikisha leseni hiyo pasipo kuwashirikisha wananchi waliochangia fedha.
Mkuu wa Mkoa pia ametumia wasaa huo kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi mbalimbali ambapo ameagiza uongozi wa Wilaya kushughulikia kero hizo likiwemo tatizo la maji safi na salama katika maeneo hayo.
Mkuu wa Mkoa pia ameongoza harambee ya kuchangia ukamilishaji wa jingo la zahanati ya kijiji cha Musasa ambapo jumla ya shilingi Milioni 5,120,000 zilipatikana ikiwa ni fedha taslimu, vifaa, na ahadi kutoka kwa viongozi na wananchi waliokuwepo katika mkutano huo.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.