Ni katika Mkutano wa Mwaka uliowakutanisha watumiaji wa Maji ngazi ya Jamii (CBWSOs) pamoja na wadau wa Sekta ya Wadau wa Maji.
Akitoa neno la utangulizi Eng Avitus Exavery katika Mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi Mhe. Mkuu wa wilaya ya Chato Eng. Deudedith Katwale uliofanyika katika ukumbi wa Chato Beach Resort amesema " hali ya upatikanaji wa maji katika wilaya yetu ni zaidi ya asilimia 68 ambapo mpaka itakapofika 2025 tunategemea kuwa na asilimia 85 ya upatikanaji wa maji katika vijiji vyetu ambavyo vinapata maji kupitia bomba au visima ambavyo tumevichimba"
Akitoa malengo ya Mkutano huo wa mwaka Eng. Avitus amesema kupitia kikao hicho washiriki watapata fursa ya kujengewa uwezo katika nyanza za utunzaji wa nyaraka za manunuzi kutoka kwa mtaalamu wa ofisi ya Ukaguzi wa Ndani, mtu wa TAKUKURU dhidi ya vitendo vya Rushwa pamoja na Sheria za Huduma za Maji kutoka kwa wataalamu wa RUWASA.
Eng. Avitus ameongeza kwa kusema Chanzo cha fedha katika utekelezaji wa Miradi ya RUWASA ni kutoka Serikali kuu kupitia mradi wa P4R ambapo tunalipwa kutoka na matokeo ambapo kwa mwaka ujao wa fedha tumetengewa zaidi ya Bilioni 5 hivyo ni imani yangu kuwa kwa mwaka ujao wa fedha mtandao wa maji utaongezeka hasa maeneo ambayo yalikuwa hayajafikiwa, mfano Mradi mkubwa wa Maji Bwanga
Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Ndg. Christian Manunga akiongea na washiriki wa Mkutano huo amewaomba watu wa RUWASA kuendelea kuongeza kazi katika kuhakikisha kila kijiji kinapata maji mapema na haraka iwezekanavyo kwani bado kuna baadhi ya vijiji vyetu havina maji safi na salama.
Mhe. Mkuu wa wilaya ya Chato Eng. Deusdedith Katwale akiongea na washiriki wa kikao hicho amewaomba RUWASA pamaja na wadau wa sekta ya Maji kuendelea kushirikiana hasa katika kulinda na kutunza vyanzo vyetu vya maji pamoja na miradi ya maji inayotekelezwa katika maeneo yetu.
Aidha Mhe. Katwale amewapongeza watumiaji wa maji ngazi ya Jamii( CBWSOs) kwa namna ambavyo wamekuwa msitari wa mbele katika kuhakikisha miradi inayoanzishwa katika jamii inaleta tija na kuwa endelevu.
Katika hatua ingine Mhe. Katwale amewaangiza watu wa RUWASA, Afisa Mazingira na Ofisi ya Mkurugenzi Chato kuhakikisha maeneo ambayo yameharibiwa na kupoteza uoto wake hivyo upatikanaji wa vyanzo vya maji kuwa tatizo hasa maeneo ya pembenzoni kama kule Nyantiba kuona ni namna gani tunarudisha hali ya uoto kama ilivyokuwa hapo mwanzo.
Katika hatua nyingine Mhe. Mkuu wa wilaya amekabidhi vyombo vya usafiri na vitendea kazi venye thamani ya zaidi shilingi milioni 30 ambavyo ni Pikipiki, Guta pamoja na Kompyuta kwa wasimamizi wa huduma za maji ngazi ya jamii katika Kata za Bwongera, Mganza, na Kigongo wamepata pikipiki 2, Guta 1 na Kompyuta1 pia Makurugusi na Ilemela pikipiki 2 na Kata ya Iparamasa imepokea pikipiki 2 na Kompyuta mpakato 1
Kwa upande wa Wahe. Madiwani kutoka katika kata zinazotekeleza miradi ya mbalimbali ya RUWASA ndani ya Halmashauri wamemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia S. Hassan kwa namna ambavyo amezidi kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wairadi ya Maendeleo ndani ya Halmashauri hasa katika utekelezaji wa Miradi ya Maji.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.