Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chato Ndg. Mandia Kihiyo akitoa neno kabla ya kumkaribisha Mhe. Mkuu wa wilaya ya Chato amewashukuru wananchi wote waliojitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani ambayo kiwilaya yamefanyika katika kijiji cha Msasa katika Kata ya Makurugusi.
Ndg. Mandia amesisitiza wanawake kuwa msitari wa mbele kwani anaamini kuwa wanawake ni Jeshi kubwa katika kila hatua kwa mfano katika shughuli za uzalishaji, maendeleo ya kaya na familia kwa ujumla.
Pia ameongeza kwa kusema leo katika maadhimisho haya Halmashauri ya Chato itatoa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 107 ikiwa ni ongezeko la milioni 32 toka kiwango kilichotolewa mwaka 2022 katika maadhimisho haya.
Mhe Mkuu wa wilaya ya Chato akitoa hutuba yake kabla ya kukadhi mikopo hiyo amewataka akina mama wa chachu kuona fursa mbalimbali kulingana na maeneo yanayowazunguka, ameongezwa kwa kusema Kauli mbiu hii ya Maadhimisho ya Mwaka huu 2023 haikuja kwa bahati mbaya " Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia; chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia"
Mhe. Joseph Katwale amebainisha hayo kwa kuwataka wanawake wote kuwa msitari wa mbele katika kutumia fursa za mabadiliko ya teknolojia katika kujiletea maendeleo hasa katika nyanja za kilimo, ufugaji na hata katika biashara.
Aidha Mhe. Mkuu wa wilaya amewataka viongozi kuanzia ngazi ya Kata na kijiji kuhakikisha watoto wote wanafika shuleni hasa watoto wa kike na kuondokana na dhana potofu dhidi ya kumwelimisha mtoto wa kike, pia amekemea tabia ya baadhi ya vikundi kukopa fedha hizi zitokanazo na mapato ya ndani ya Halmashauri kurejesha haraka iwezekanavyo na niseme wazi tu hapa tutachukua hatua kali kwa wahusika wote, 'Mkurugenzi naomba niipate ofisi taarifa ya vikundi vote vilivyokopa fedha'
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.