Uongozi wa chama cha Skauti Wilaya ya Chato, wameishukuru Serikali kupitia viongozi wa Wilaya hiyo kuwaruhusu vijana zaidi ya 200 wa Skauti kutoka shule zote za Sekondari na Msingi (W) kuweka kambi ya kielimu na jukwaa la vijana ikiwa ni maandalizi ya Mapokezi ya Mwenge wa uhuru wilayani humo, waliyoiweka katika shule ya Msingi Magufuli iliyopo Kijiji cha Mlimani kata ya Muungano.
Kambi hiyo ilidumu kwa siku tatu ambapo ilianza Agosti 15 - 17, 2025 huku ikiongozwa na Kamishna wa Skauti ngazi ya wilaya Novati Msipa Underson (DSC - Chato) ikiwa na lengo maalumu la kuwaandaa vijana wa Skauti kushiriki kikamilifu mbio za Mwenge wa uhuru wilayani humo ifikapo 06, 09, 2025 katika vipengele vya Hamasa, paredi ya itifaki ya Skafu wakati wa mapokezi ya Mwenge pamoja na maandalizi ya vijana wa skauti watakao shiriki kambi ya Kielimu na mashindano Mkoa wa Geita kuanzia 22 - 24, 08, 2025.
Kamishna Msipa amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Chato kwa ushirikiano mkubwa walioufanya kuhakikisha wanapata huduma muhimu kwa muda huo wa siku tatu vijana hao wamekumbushwa suala la ukakamavu na mafunzo ya kuwajengea uimara wakati wa zoezi muhimu la Kitaifa la mapokezi na kukimbiza Mwenge ndani ya wilaya hiyo ikiwa ni sambamba na kuwapa elimu juu ya Falsafa ya Mwenge wa Uhuru hapa nchini.
"Kutoka Moyoni sisi Vijana wa Skauti Wilaya ya Chato tunaipongeza Serikali kupitia Viongozi wa Wilaya ya Chato kwa ushirikiano mkubwa na ukarimu waliotuonesha kwa siku tatu tulizokaa kambi katika Shule ya Msingi Magufuli eneo ambalo vijana wamepata elimu ya kutosha dhidi ya ukakamavu, uzalendo, Falsafa ya Mwenge wa uhuru sambamba na kuwakumbusha kuzingatia suala la nidhamu na utiifu. Alisema Kamishna Msipa"
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.