Fedha hizo zimetolewa na TASAF (Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini) kupitia Mradi wa Kuinua Uchumi wa Kaya amabapo katika Halmashauri ya Chato mradi huo unatekelezwa katika vijiji viwili ambayo ni kijiji cha Mnekezi kata ya Iparamasa na kijiji cha Nyakato kata ya Bukome.
Katika Mradi huo wa kuinua uchumi wa kaya, vikundi 10 venye kaya 133 vimepokea mbuzi 399 na kila kaya imepokea mbuzi 3 ambapo kila kaya inapata dume 1 na majike 2.
Pia Mradi huo umetoa madawa pamoja na vifaa tiba kwa ajili ya kuhakikisha mifugo hao waliogawiwa kupitia mradi huo wanakua vizuri na kuwa na afya bora ili lengo la mradi liweze kutimia.
Akizungumza na walengwa wa TASAF katika mradi huo Bi. Aisha Kesowani amewataka Ma Afisa Mifugo katika vijiji husika kuhakikisha wanakuwa na ratiba ya kutembelea walengwa katika kaya zao lengo ikiwa ni kuhakikisha wanakuwa na elimu ya kutosha juu ya ufugaji wa mifugo hiyo na niwe muwazi, twendeni "tukawatunze mbuzi kwani wanapoongezeka hiyo ni mali yako"
Kwa upande wa Afisa Maendeleo ya Jamii Bw. Godfrey Nyamko amewataka kila kikundi kuzingatia mafunzo waliyopatiwa juu ya mradi huo hasa juu ya ufugaji bora wa mbuzi na matunzo yake.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Iparamasa amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya Mradi wa kuinua uchumi wa Kaya kupitia mpango ufugaji Mbuzi katika kijiji chake na hivyo kumuahidi kuwa watashirikiana na Serikali ya kijiji na wataalamu ndani ya kata kuhakikisha mbuzi hao pamoja na vifaa tiba vilivyotolewa vinatumika kama ilivyokusudiwa na mradi huko akitoa onyo kali kwa yeyote atakae fanya hujuma katika mradi huo.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.