Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Chato Ndugu Mandia Kihiyo amesisitiza uwajibikaji wa pamoja katika kuhakikisha lishe bora inapatikana.Akiongoza kikao cha kamati ya lishe ya Wilaya amesema ni wajibu wa kila mmoja kushirikiana na kitengo cha lishe.
“Lishe ni muhimu sana,tuna wajibu wa kuhakikisha watoto wote wanapata lishe bora.Tutoe elimu kwenye vituo vya afya juu ya vyakula muhimu ili kupinga vita utapiamlo Chato” amesema Kihiyo.
Ameongeza kuwa kila idara ina wajibu katika kuchangia kukuza lishe. “Afisa Elimu ahakikishe shule zina bustani za mboga mboga na kupanda miti ya matunda. Afisa Kilimo atoe ushauri wa kitaalamu juu ya aina nzuri za mbegu kwaajili ya matunda na wananchi waelimishwe juu ya umuhimu wa kula makundi yote ya vyakula hasa kuzingatia ulaji wa protini ili watoto wapate lishe sahihi”.
Utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa robo ya Oktoba - Disemba 2024/2025 umetekelezwa katika kiwango kinachotakiwa kwa viashiria vyote kupata asilimia zaidi ya 90 na kuimarika kwa matibabu ya watoto wenye utapiamlo katika hospitali ya Wilaya.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.