Kutoka na zoezi linaloendelea la mfumo wa anuani za Makazi na Postikodi katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania, vijana wa kata ya Muganza Wilayani Chato wananufaika na mfumo huo kwa kujipatia kipato kwa kuandika namba za nyumba kwa kutumia vibao maalumu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, vijana hao wamesema kwa sasa wamekuwa wakijipatia fedha kati ya shilingi elfu 50 hadi shilingi laki 3 kwa siku kutokana na utengenezaji wa vibao hivyo vya kubandika kwenye nyumba ambavyo vimekuwa vikitengenezwa kwa gharama ya shilingi elf moja.
"Mimi nilikuwa naendesha boda boda lakini kutokana na gharama za mafuta kupanda nimeamua nigeukie kipaji changu cha uchoraji, kwakweli huku napata fedha isiyopungua elf 50 kwa siku kutengeneza vibao hivi" amesema Peter Misalaba mmoja wa watengeneza vibao waliopo mjini Muganza.
Kwa upande wake mtendaji wa kijiji cha Katemwa James Kongwa amesema katika kijiji hicho kuna jumla ya kaya 800 zilizosajiliwa ambapo hadi sasa kaya zaidi ya 400 zimebandika namba za makazi ambapo amesema kutokana na vijana hao kujitokeza kutengeneza namba hizo kumeongeza hamasa ya wananchi kutengeneza vibao hivyo.
=======Mwisho======
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.