Umoja wa vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana (Hisa) vilivyopo kata ya Muganza Wilayani Chato vimetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima wanaosoma katika shule ya Awali na Msingi ya Bin Ghanim iliyopo kata ya Bwanga.
Akikabidhi vifaa hivyo Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Chato ndugu Vicent Bushaija amevipongeza vikundi hivyo kwa kutoa sehemu ya fedha zao ili kusaidia watoto hao ambapo amewataka kuendeleza moyo huo wa upendo kwa makundi maalumu yenye uhitaji.
"Kwa vikundi tulivyonavyo katika Wilaya yetu vingekuwa na utaratibu kama wa kwenu basi tungeweza kufika mbali, na tungepunguza utegemezi kwenye makundi maalumu" amesema ndugu Bushaija.
Katika Hatua nyingine ndugu Bushaija ameyapongeza mashirika ya shirika ya Plan International na SEDT kwa usimamizi mzuri wa vikundi hivyo na ushirikiano mzuri uliopo baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato na Mashirika hayo ambapo amesema ushirikiano huo ndio umeweza kutoa vikundi ambavyo vinarudisha faida kwa jamii kwa kutoa sehemu ya michango yao.
Meneja wa Shirika la Plan International Mkoa wa Geita ndugu Aldoph Kaiondoa amevipongeza vikundi hivyo na kutaka vikundi vingine viige mfano huo wa kurudisha kwa jamii hususan wenye uhitaji.
Ndugu Kandoa amepongeza pia ushirikiano mzuri ulipo baina ya Halmashauri na shirika la Plan International kwani mambo mengi yanafanikiwa ni kutokana na mahusiano mazuri.
Mwenyekiti wa vikundi hivyo ndugu Mauli Charles amesema wameamua kutoa sehemu ndogo ya fedha kwa ajili ya kutoa msaada kwa yatima hao ili kuwakumbuka yatima utaratibu ambao utakuwa ni endelevu.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na sare za shule, Sabuni, Sukari, Madaftari, Kalamu, Mchele, Mahindi vyote vikiwa na thamani ya shilingi laki 6.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.