Jumla ya nyumba sita ambazo zimejengwa na serikali kwa ufadhili wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) shule ya sekondari Ilemela zinatarajia kuboresha makazi ya walimu.
Nyumba hizo ambazo zimejengwa kwa gharama ya shilingi 152,000,000 zinatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2019 na kuanza kutumika.
Kukamilika kwa nyumba hizo kutapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la uhaba wa nyumba kwa walimu wa shule ya sekondari Ilemela iliyopo kata ya Ilemela.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Eliurd Mwaiteleke emesema Halmashauri ya Wilaya ya Chato itaendelea kufanya juhudi za kutafuta wafadhili ili kuendelea kuboresha makazi ya walimu kwa shule zote za sekondari na zile za msingi. Halmashauri ya Wilaya ya Chato ina shule za sekondari 25 na 152 za msingi.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.