Mkuu wa Wilaya ya Chato mhe. Shaaban Ntarambe ameagiza kukamatwa na kuwekwa Mahabusu baadhi ya wanafunzi wanaopata mimba na kuficha ushaihidi wa wahusika wa mimba.
Agizo hilo amelitoa wakati akiongea kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa tarafa ya Buseresere.
Amesema kumeibuka tabia ya baadhi wanafunzi wanaopata ujauzito kudanganya kwa lengo la kupotezea ushahidi pindi wanapofikishwa kwenye vyombo vya sheria na kusababisha wahusika kutokuchukuliwa hatua za kisheria
"Hili la mimba watu mnafanya mzaha, watu wazima wanaoa wanafunzi... kuanzia sasa suala la mimba Chato tutataka liwe historia, wasichana hawa pia wamekuwa wakorofi akitiliwa mashaka na atakayegundulika na mimba kwenye upimaji ule wa kila baada ya miezi miwili weka mahabusu kwanza saa 24 abanwe mpaka aseme aliyempa mimba" Alisema Mkuu wa Wilaya
Mkuu wa Wilaya amemwagiza Mkuu wa jeshi la polisi Wilaya ya Chato kushirikiana na Serikali za vijiji kutekeleza agizo hilo mara moja
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ameonya tabia ya utoro kwa wanafunzi na amewataka wazazi kushirikiana na jamii kila mmoja ashiriki kuzuia utoro.
Ameagiza wanafunzi wote ambao bado hawajaandikishwa wapelekwe wakaandikishwe mara moja kuanzia sasa hata kama hawana sare za shule.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.