Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe. Said Nkumba,April 23,2024 akiendelea na ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwa ni katika kutekeleza ratiba ya matukio ya kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kiwilaya, pia amezindua chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wa miaka 9 hadi 14.
Uzinduzi huo umefanyika Shule ya Sekondari Chato, ukihudhuliwa na ofisi ya Mkuu wa wilaya, timu ya menejimenti,wataalamu wa chanjo,wanafunzi wa kidato cha 1 - 4 na baadhi ya walimu wa shule hiyo, ambapo kiwilaya wanatarajiwa kuchanjwa wasichana 55,806 kati yao miaka 9 ni 10,422 na miaka 10 - 14 ni 45,384, shule za msingi 169 na Sekondari 55.
"Chanjo hii ni salama na itawafanya kuwa na afya bora na uzazi ulio salama pindi watakapokua wakubwa,hivyo nawasihi wazazi na walezi tuwakinge watoto wetu kwa kuhakikisha wanapata chanjo ili kuepuka ugongwa huu hatari wa saratani ya shingo ya kizazi,nawaasa wapuuzeni wapotoshaji" Alisema Nkumba
Kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Chato Ndg Elibariki Mollel amesema maandalizi yapo vizuri,timu zote za kukamilisha zoezi la chanjo wamepatiwa mafunzo, uhamasishaji unaendelea, chanjo na vifaa vingine vimesambazwa kwenye vituo vinavyotoa huduma, na kuongeza kuwa chanjo hii ni kuanzia 22 - 28/04/2024.
Ziara hiyo pia ilikagua mradi wa upanuzi wa shule ya Sekondari Ichwankima ili kupokea kidato cha 5&6 wenye thamani ya Tsh. 919,425,000/= kwa majengo ya madarasa 4, maktaba,nyumba ya watumishi 2 in 1, Utawala, mabweni 2,bwalo,vyoo, pamoja na maabara ambapo Mhe. Nkumba alikiri kufurahishwa na mshikamano uliopo kwa viongozi kusimamia ujenzi kwani matokeo yanaonekana hatua za mradi nzuri na viwango vya ubora kuzingatiwa.
Aidha alikagua na kuweka jiwe la msingi Zahanati ya kijiji cha Mwekako iliyogharimu Tsh - 54,962,500/= ikiwa nguvu za wananchi 36,882,500/=, mfuko wa jimbo 1,200,000/= na mdau wa maendeleo (Hellenor Foundation) 16,879,800/= pamoja na vifaa tiba vyenye thamani ya 3,955,000/= ambavyo ni vitanda vya wagonjwa 2 na chakujifungulia1, 2,magodoro 2,Pazia la blue,mzani wa watu wazima,mzani wa watoto,Baiskeli ya wagonjwa
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.