Wilaya ya Chato ina jumla ya Shule za Sekondari za kidato cha tano na sita 09 zenye mikondo 56, watahiniwa 2234 ambapo kati yao ME 1163 na KE 1071 huku waliosajiliwa mchepuo wa Sayansi wakiwa ME 357, KE 254 jumla 611 wakati waliosajiliwa mchepuo wa Sanaa ME 806 KE 817 jumla 1623 wanaotarajia kuanza mitihani yao ya kuhitimu kidato cha sita Mei 5, 2025.
Afisa Elimu Sekondari (W) Mwl Longino Ludovick amezitaja shule hizo kuwa ni Buseresere, Ilemela, Jikomboe, Janeth Magufuli, Muungano Boys, Zakia Meghji, Bwina, Chato pamoja na Magufuli Sekondari ambapo amebainisha kuwa shule zote 09 ni za Serikali hakuna shule za binafsi.
Ludovick ameeleza kuwa walimu wametimiza majukumu yao kikamilifu kwa kuwafundisha watahiniwa na kumaliza mada mapema ikiwa ni pamoja na kuwapa mazoezi ya kutosha ili kuwajengea umahiri utakao wasaidia kujibu mitihani yao vizuri.
Mkurugenzi Mtendaji (W) Ndg Mandia Kihiyo amekiri kuwa maandalizi ya Mtihani yamekamilika kwa kuwapatia
mafunzo na maelekezo ya kina wasimamizi wote wa mitihani lengo likiwa ni kuhakikisha kazi inafanyika kwa ufanisi unaotarajiwa.
"Walimu wote watakao simamia mitihani wamepewa semina elekezi na wameandaliwa vizuri kufuata mwongozo wa baraza la Mitihani pamoja na vyombo husika vinavyounda kamati ya mitihani, ulinzi na usalama upo imara kuhakikisha kazi inafanyika kwa usalama wa hali ya juu bila udanganyifu" Alisema Kihiyo.
Aidha Ndg Kihiyo amewatakia mtihani mwema watahiniwa wote wa kidato cha sita 2025.
Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kupitia baraza la Mitihani la Tanzania imetoa ratiba ya mtihani wa kidato cha sita mwaka 2025 kuwa unatarajia kuanza Mei 05 na kuhitimisha Mei 26, 2025.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.