Akifungua Mkutano kati ya Timu ya Menejimenti pamoja na Watendaji wa Vijiji uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Chato Kaimu Mkurugenzi Bw. Geraid Mgoba ambaye ni Afisa Kilimo na Uvuvi wilaya akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji Bw. Mandia Kihiyo amewataka watendaji wa vijiji kuwa msitari wa mbele katika ukusanyaji wa mapato kwani vyanzo vyote vipo katika maeneo yao.
Ambapo amewataka watendaji hao kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha makusanyo yanapatikana na yanakusanywa kwani kama Halmashauri tumekusanya asilimia 29.57 na tulitakiwa ifikapo 31 Disemba 2022 tuwe tumekusanya asilimia 50 lakini kiasi kilichokusanywa ni asilimia 29.75 tu sawa na shiling 1,299800,203.80 ya bujeti ya Halmashauri ambayo ni 4,395,600,000
Akichangia mada mtendaji wa kijiji cha Buseresere amemwomba Mweka Hazina wa Halmashauri kuangalia namna ya kuweka utaratibu wa kutoa motisha kwa viongozi hao hasa wanapokuwa katika shughuli za kusimamia ukusanyaji wa mapato ikiwa ni pamoja na kuwalipa kwa wakati asilimia 5
Nae Mtendaji wa kijiji cha Iparamasa akichangia mada amesema yeye katika mnada wake anachangamoto ya miundo mbinu jambo ambalo linachangia kwa kiasi fulani mapato kuwa chini, amabapo kwa sasa anakusanya kiasi cha shilingi 120,000 hadi 350,000 hata hivyo amehaidi kuongeza zaidi ukusanyaji kwa kubana mianya yote ya ukwepaji katika ulipaji wa mapato ndani ya mnada wake.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu Bw. Edward Malima akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wajumbe wa mkutano huo amesema, mimi pamoja na ofisi yangu tumejipanga kuhakikisha kila anaedai stahiki yake basi analipwa kwa wakati lakini ombi letu ni moja tu ndugu zangu twendeni tukakusanye mapato ili kila mmoja wetu apate haki yake'
Ameongeza Bwn. Malima kuwa Mapato katika Halmashauri ndo uti wa mgongo kwani hakuna Halmashuri bila mapato.
Akihitimisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Bw. Mandia Kihiyo amewaasa watendaji wa vijiji kuwa wabunifu katika dhana nzima ya ukusanyaji wa mapato kwani zoezi la ukusanayaji mapato siku zote toka kuumbwa kwa ulimwengu halijawahi kuwa la hiari hivyo watendaji wote katika kijiji na kata shirikianeni kwa pamoja lengo mapato yote ndani ya kijiji yanakusanywa.
Pia amewaasa watendaji kuwa na nidhamu na uaminifu katika kutoza viwango sahihi toka kwa wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali katika maeneo yao.
Mwisho amewataka watendaji wa vijiji kuhakikisha kila mmoja anatoa elimu kwa wananchi wake juu ya umhimu wa kujiunga na Bima ya Afya ya CiHF na kuhakikisha walau kila mtendaji kuhakikisha amesajili wanacha 50 kila mwezi, ambapo kila kaya itaundwa na watu 6 kwa kiwango cha shilingi 30,000
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.