Wilaya ya Chato inatarajia kutoa Chanjo kwa watoto 217,500 ifikapo tarehe 04 Disemba 2022 ikiwa ni Awamu ya Nne ya utoaji wa Chanjo ya Polio, ambayo hutolewa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 05.
Ameyasema hayo Mhe. Mkuu wa wilaya ya Chato Bi. Martha Mkupasi wakati wa uzinduzi wa utoaji wa Chanjo hiyo katika kijiji cha Nyatimba kata ya Nyarutembo.
Aidha amewaasaa wananchi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kupata chanjo hiyo kwani mtoto akipatwa na ugonjwa huu hupooza viungo vya mwili wake na hivyo kushindwa kujihudumia na kuwa tegemezi kwa familia na jamii nzima inayomzunguka maisha yake yote
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.