Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato ambaye ndiye Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ndg. Geriad Mgoba, Agosti 25, 2025 alifanya kikao na watumishi wapya wa idara ya kilimo chenye lengo la kuwataka kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa wanapowahudumia wananchi ili kutimiza haja ya Serikali kwani imewekeza rasilimali nyingi kuwaajiri wataalamu ili wananchi wapate huduma iliyo bora na kuongeza uzalishaji.
Akizungumza na watumishi hao Ofisini kwake aliwasisitiza wataalamu hao kuhakikisha wanakuwa chachu ya kuleta matokeo chanya katika Sekta ya kilimo kwa vitendo kwenye maeneo yao ya kazi kwa kutoa ushauri wa kitaalamu na kufuatilia utekelezaji wake.
" yetu ni ya vitendo, hivyo nendeni mkafanye kazi na matokeo yaonekane kwa kuongeza uzalishaji, Serikali imewekeza kwa kuwapa ajira na lengo lake wananchi wahudumiwe na kupitia ninyi Sekta ya kilimo ikakuze kipato chao, mkaitumie vizuri taaluma yenu kwa kutoa ushauri wa kitaalamu na kufuatilia matokeo yake, lakini pia mshirikishane ninyi kwa ninyi katika kutoa huduma bora kwa wananchi ili waweze kulima kilimo chenye tija na kuwanufaisha"Alisema Mgoba
Aidha Mgoba aliipongeza Serikali kwa kuajiri watumishi wengi wa kada mbalimbali huku akizungumzia idara ya kilimo kuwa anaozungumza nao waliajiriwa 13 Mwezi Julai 2025 na kabla ya hapo idara ilikuwa na maafisa kilimo 93 walio chini ya halmashauri na Mhandisi wa Umwagiliaji 01aliye chini ya Tume ya Umwagiliaji hivyo ongezeko hilo la ajira mpya linapelekea wilaya kuwa na Jumla ya maafisa kilimo 106 waliopo wilayani Chato.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya utawala na usimamizi wa rasilimali watu wa halmashauri ya wilaya hiyo Bi. Sarah Charles amewataka kufanya kazi kwa uadilifu, weledi na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma katika utekelezaji wa majukumu yao huku akiwasisitiza suala la mavazi ya kiutumishi.
Pamoja na yote pia walipata fursa ya kujifunza mifumo mbalimbali ya kiutumishi na ya kiutendaji kama vile PEPMIS (e _ Watumishi), M- KILIMO, ARDS, kusajili wakulima,pamoja na Upimaji wa udongo,
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.