Waziri Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi wa mabweni kwa ajili ya kuanza kwa kidato cha tano na sita shule ya sekondari Bwina iliyopo Chato
Baadhi watumishi wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wakimsikiliza Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo la Chato Mhe. Dkt. Medard Kalemani
Waziri wa nchi ofisi ya Rais- TAMISEMI Selemani Jafo akiongea na watumishi wa Halmashauri kwnye ukumbi wa mikutano
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Selemani Jafo amesema watumishi wazembe waliopo Halmashauri ya Wilaya ya Chato hasa wakuu wa idara wabadilike kuanzia sasa na si kuhamishwa vituo vya kazi.
Waziri Jafo amesema hayo leo wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Chato kwenye ziara yake ya siku moja Wilayani hapa.
”Wakuu wa idara fanyeni kazi, saidianeni, fanyeni kazi kama timu, ondoeni ubinafsi katika kazi ili kuleta mabadiliko hapa Chato… lakini wale watakaoshindwa kujirekebisha kuanzia leo hatutawahamisha bali tutawashusha vyeo mara moja” amesema Waziri Jafo.
Waziri Jafo amesema kutokana na mabadiliko ya viongozi yaliyotokea Wilayani Chato, anatarajia shughuli mbalimbali zitatekelezwa vizuri na kwa wakati ambapo amewataka watumishi kuwapa ushirikiano viongozi hao.
Waziri Jafo pia amewataka wakuu wa idara katika maeneo mbalimbali nchini kufanya kazi zao kwa kujiamini na kuacha kushinikizwa na wanasiasa ambao wamekuwa chanzo cha kuvuruga shughuli mbalimbali hususan fedha zinazopelekwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri Jafo katika ziara yake ametembelea shule ya Sekondari Buseresere ambapo amesema serikali italeta fedha shuleni hapo kiasi cha Shilingi milioni 250 kwa ajili ya uanzishaji wa kidato cha tano na sita shuleni hapo na amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chato Eliurd Mwaiteleke kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ifikapo Februari 2019.
Maeneo mengine yaliyotembelewa na Waziri Jafo ni pamoja na Ujenzi wa sekondari ya Minkoto, Zahanati ya Mutundu ambayo ameagiza utaratibu wa kuipandisha hadhi na kuwa kituo cha Afya uanze, Ujenzi wa sekondari ya kidato cha tano na sita sekondari ya Bwina ambapo pia ameagiza wizara ya elimu kuhakikisha inapeleka wanafunzoi wa kidato cha tano ili shule hiyo iweze kuanza mapema, ujenzi wa sekondari ya Kikumbaitale na Zahanati ya kata ya Ilemela ambayo inapandishwa hadhi na kuwa kituo cha afya na ujenzi wake utaanza mapema mwezi huu.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.