Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameitaja mikoa ya Tabora, Geita, Mtwara na Shinyanga kuwa inaongoza kwa utoro wa wanafunzi wa sekondari.
Waziri mkuu pia ameitaja mikoa ya Rukwa, Geita, Tabora, Singida na Simiyu kuwa inaongoza kwa utoro wa wanafunzi wa shule za msingi.
Waziri Mkuu ameitaja mikoa hiyo leo wakati akizindua mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Magogo mkoani Geita.
Mbio za Mwenge zitakazohitimishwa Oktoba 14,2018 mkoani Tanga zinaongozwa na kauli mbiu “Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya nchi yetu.”
Majaliwa amesema Mkoa wa Tabora unaongoza kwa asilimia 9.7 ya wanafunzi watoro wa sekondari ukifuatiwa na Geita (asilimia 8.1), Mtwara (asilimia 6.1) na Shinyanga (asilimia 6.3).
Kwa shule za msingi, Rukwa inaongoza kwa asilimia 3.2, ukifuata Geita (asilimia 3.1), Tabora (asilimia 2.9), Singida (asilimia 2) na Simiyu (asilimia 2).
“Kwa jumla utoro wa wanafunzi wa sekondari ni mkubwa kuliko shule za msingi. Naikumbusha mikoa yote niliyoitaja kuhamasisha wananchi wakiwamo wazazi na walezi kuhusu umuhimu wa elimu na mahudhurio endelevu shuleni kwa kutumia utaratibu wa sheria zilizowekwa,” amesema Majaliwa.
Naye Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jensita Mhagama ameelezea kuwa mwenge ni Chombo kilichoasisiwa na Baba wa Taifa ,Mwl Julius Kambarage Nyerere Mwaka 1961 ikiwa ni tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika.
“Mbio za mwenge wa uhuru zilianza rasmi mwaka 1964 baada ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar uliozaa nchi inayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”Alisema Waziri Jenista.
Mwenge wa uhuru utakimbizwa katika mikoa yote 31 ya Tanzania katika halmashauri 195 na kwa muda wa siku 195.
Sherehe hizo zilizosindikizwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma za asili, kwaya, na halaiki zilifana huku zilihuidhuriwa na wakazi wengi.
Huku kauli mbiu ya Mwenge wa mwaka huu ikiwa ni” Elimu ni ufunguo wa maisha ,wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa”
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.