TAARIFA FUPI YA MRADI WA KIWANDA CHA KUSINDIKA ZAO LA ALIZETI
CHATO AMCOS
Katika harakati za kuongeza kipato cha wananchi wa wilaya ya Chato Halmashauri ya wilaya ilifanya uhamasishaji kwa wakulima kuanza kuzalisha zao la alizeti kwa msimu wa 2013/2014. Baada ya wananchi kuitikia halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tuliweza kuanzisha viwanda vidogo 6 vya kusindika mafuta ya alizeti katika kata za Bwongera, Kigongo, Minkoto, Busereserena Chato ikiwemo kiwanda hiki cha Chato AMCOS. Kiwanda hiki cha Chato AMCOS kiliendelea kufanya kazi ya kusindika mafuta ya alizeti yanayochujwa maramoja.Mwaka 2014 Chato AMCOS ilitembelewa na Balozi wa Japan nchini Tanzania na kuahidi kuwapatia msaada wa mtambo wa kusafisha mafuta ya alizeti kwa mara ya pili (double refinery).
Mnamo tarehe 20/03/2015 Halmashauri ilipokea kiasi cha Tsh 170,919, 858.00 kwa ajili ya kutekeleza mradi huu. Kwahiyo, mradi huu unatekelezwa kwa ufadhili wa Ubaloziwa Japan Tanzania kupitia mpango wake (GRANT ASSISTANCE FOR GRASS - ROOTS HUMAN SECURITY PROJECT) ambao umetoa jumla ya Tshs. 170,919,858/= kwa ajili ya utengenezaji wa mitambo na kuisimika.Halmashauri imechangia Tshs. 25,000,000/= Kwa ajili ya ukarabati wa ghala la kusimika Mashine.
Utekelezaji:Halmashauri iliingia mkataba na SIDO Mkoa wa Shinyanga kununua, kutengeneza na kusimika mashine kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda hiki tarehe 13/03/2015 kwa kipindi cha miezi 6 kwa thamani ya Tshs. 164,650,000/=. Kwa upande wa ukarabati kutokana na upatikanaji wa fedha kutokuwa mzuri Halmashauri iliamua kukarabati kwa kutumia usimamizi wa wataalam wake ofisini.
Hadi leo hii kwa upande wa SIDO Mkoa wa Shinyanga wa meleta Mtambo wa Double Refine, Boiler, Mashine ya kukamua na kuchuja mafuta,mashine ya kuondoa mchanga na uchafu kwenye mbegu za Alizeti(Distoner) na tayari tumeshawalipa Tshs. 63,700,000/=.Kazi ya ununuzi na usimikaji Mashine ya kufungasha mafuta imeishafanyika na tayari majaribio ya awali ya Mtambo wa double refine yamefanyika na matokeo yake ni ya kuridhisha.
Kwa upande wa ukarabati wa ghala jumla ya Ths. 19,807,500/= zimetumika kwa kuezeka bati, kujenga kuta na kubadilisha ngu zozilizokuwa mbovu, ujenzi wa ngazi na banda la kuuzia mafuta na kurudishia bati za ukutani. Kazi zilizosalia ni kupaka rangi, kukamilisha ofisi ya ndani na banda la kuuzia mafuta, kusawazish aeneo la mbele la kiwanda na kuweka vigae kwenye ngazi ambazo zinatarajiwa kugharimu jumla ya Tshs. 5,000,000/=.Ukamilishaji wake umechelewa kutokana na upatikanaji wa fedha za makusanyo ya ndani kutokuwa wakuridhisha.
Mradi huu ukikamilika utaweza kuajiri wa kazi wa Chato hususani ni vijana wasiopungua 30 kwa ajili ya Matengenezo ya kawaida na uendeshaji kwenye maeneo ya uzalishaji na masoko. Uwezo wa kiwanda utakuwa ni kilo 2,400 kwa masaa 8, zitakazotoa lita 686 na mt ambo wa refinery unauwezo wa kuchuja mafuta lita 500 hadi kupaki kwa masaa 5.
Mpango wa Halmashauri ya Wilaya ni kukabidhi mradi kwa Chama cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato kwa hati ya makubalino juu ya Umiliki na Uendeshaji kwa manufaa ya wanachama na jamii kwa ujumla chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Wilaya kwa lengo la kuhakikisha kuwa Mradi unaendelea kuwa endelevu.
Chama cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato nimiongoni mwa Vyama 30 vilivyondikishwa katika daftari la Vyama Vya Ushirika Nchini kwa namaba ya usajiri KAR 388. Chama hiki kinao jumla wanachama 146 (Wanaume 112 nawanawake 34). Aidha kina miliki Maghala 3, Vibanda vya biashara 56 vilivyojengwa kwa ubia na wafanyabiashara, matenki 2 ya kisima cha mafuta, Mashine 2 za kusaga nafaka na eneo hili lenye ukubwa wa takriban ekari 1.
Halmashauri kabla ya upanuzi wa mradi huu, kupitia ASDP I tuliwawezesha kuanzisha mradi huu wa kusindika zao la Alizeti kwa kununua na kusimika mashine 1 ya kukamua na kuchuja mafuta ya Alizeti kwa thamani ya Tshs. 17,272,000/=. Ambapo Halmashauri ilitoa Tshs. 15,750,000/= na Chato AMCOS walichangiaTshs. 1,522,000/=. Mradi huu umeendeshwa kwa misimu3. Msimu 2013/14 wakulima walileta Alizeti na kukamua kilo 6,157, Msimu 2014/15 wakulima walileta Alizeti na kukamua kilo 67,873 na msimu 2015/16 wakulima walileta Alizeti na kukamua kilo 47,322.Wastan wa uzalishaji kwa gunia la kilo 70 ni lita 20 za mafuta baada ya kuchuja na mashudu kilo 35. Hivyo kwa kipindi chote cha misimu mitatu jumla ya lita 34,672 zimekamuliwa na kuzalisha mashudu kilo 60,676.
Mapato yaliyotokana na ukamuaji kwa gharama ya Tshs. 150 kwa kilo kwa kipindi ikinachoishia Aprili 30, 2016, ni jumla ya Tshs. 19,671,000/=na gharamaza uendeshaji zikiwemo matengenezo ya mashine, malipo ya watumishi, biliyaumeme, maji,leseni,matengenezo ya mizani na Malipo ya kodi ya Mapato ni Tshs. 15,290,650/=na ziada iliyo baki Tshs 4,380,950/=ambayo sehemu ya ke imeendelea kuwekezwa katika upanuaji wa mradi huu kama sehemu ya mchango wa wakulima.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.