Halmashauri ya Wilaya ya Chato katika mwaka wa fedha 2018/2019 kwenye vipaumbele vyake ilipanga kuanzisha miradi mipya ya kwa lengo la kuongeza kiwango chake cha mapato ya ndani ili kuweza lukidhi matarajio yake ya utoaji wa huduma kwa wananchi.
Kupitia maandiko mbalimbali yalipelekwa Ofisi ya Rais–TAMISEMI timu ya Menejimenti ya Halmashauri ili ainisha miradi kadhaa ikiwemo viwanda vikubwa na vya kati ili kuongeza uwezo wa Halmashauri kujitegemea kiichumi.
Miradi ambayo ilifanikiwa na kupata fedha ni kiwanda cha ufatuaji wa Matofali kilichopo kijiji cha Muungano na Uchapishaji uliopo kijiji cha Kitela kata ya Chato.
Jumla ya fedha iliyotolewa kwa miradi hii miwili ilikuwa ni shilingi 305,712,110.
Kupitia miradi mipya hiyo ambayo imeanza uzalishaji tangu mwezi Machi 2019 Halmashauri ya Wilaya ya Chato inaelekea kupata ufumbuzi wa tatizo la muda mrefu la utoshelevu wa mapato ya ndani ya Halmashauri.
Mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ikupia vyanzo vya ndani hadi kufikia mwezi Juni 2018 ilikusanya kiasi cha shilingi 1,956,905,535.45 sawa na 90.65% ya lengo la 2,158,800,000.
Kwa mwaka wa fedha 2018/2019 hadi kufikia tarehe 31 Machi 2019 Halmashauri kupitia vyanzo vya ndani imekusanya kiasi cha shilingi 1,572,278,292.09 Sawa na 69.36% ya lengo la shilingi 2,266,934,000.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Eliurd Mwaiteleke amesema kuanza kwa miradi hiyo ni dalili ya kwamba kwa mwaka 2018/2019 mapato yatakuwa ni zaidi ya asilimia 100.
“Pamoja na vyanzo vingine vya Halmashauri lakini kupitia miradi hii ya kimakakati tunatarajia makusanyo yetu ya ndani yatakuwa ni zaidi ya mwaka uliopita kwa kiwango kikubwa tu” alisema Mkurugenzi Mtendaji.
Kwa mujibu wa meneja wa kiwanda cha matofali George Philipo amesema tofali moja la nchi 6 kwa (uwiano wa mfuko mmoja tofali 40) kwa bei ya kiwandani linauzwa shilingi 1100/=.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.