Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa Mohammed Mchengerwa amefungua Kikao kazi cha Maafisa Habari wa Mikoa,Halmashauri na Taasisi za ofisi ya Rais leo 23 Mei 2025 katika Ukumbi wa Jiji Dodoma.
Akifungua kikao hicho Waziri Mchengerwa ameeleza kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI ni Wizara kubwa inayobeba asilimia karibu 21 ya bajeti kuu ya Serikali, ambapo kwa mwaka wa fedha 2025/2026 imepitishiwa bajeti ya Shilingi 11,782,984,202,00.00 zinazokwenda kutekeleza miradi kwenye Taasisi,Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
“Wizara hii ndio yenye bajeti kubwa kuliko Wizara zingine na yenye miradi mingi inayomgusa mwananchi moja kwa moja,Hivyo wajibu wenu ni kuhakikisha kazi hizi zinatangazwa vizuri na kwa takwimu sahihi “
Mheshimiwa Waziri amesisitiza kuwa Maafisa Habari ndio wenye dhamana kubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata haki yao ya msingi ya kupata taarifa sahihi na kwa wakati.Ameahidi kufanyia kazi mapungufu yaliyopo kwenye kada ya kitengo cha mawasiliano serikali na kusisitiza kuwa serikali itaongeza juhudi ya kuajiri na kuhakikisha kila Mkoa na Halmashauri inakua na Maafisa Habari.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.