SEKTA YA KILIMO
Eneo linalofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali ya Chakula na Biashara ni jumla ya Hekta 267,900 ambapo hekta zinazolimwa kwa sasa ni 99,123 sawa na asilimia 37.
Mazao Makuu ya Chakula yanayolimwa Wilayani Chato ni Mahindi, Mpunga, Mtama, Mihogo, Maharage na viazi vitamu. Mazao haya pia hutumika kama Mazao ya Biashara. Mazao Makuu ya Biashara ni Pamba, Tumbaku na Alizeti.
Mkakati wa Wilaya katika kuendeleza sekta ya kilimo kwa kuzingatia Mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa na Mapinduzi ya kijani ni kuhakikisha uwepo wa “Uhakika wa Chakula na Ongezeko la Kipato Ngazi ya Kaya”.
UZALISHAJI WA MAZAO MSIMU WA 2016/2017
Katika msimu wa Kilimo wa 2016/2017, Wilaya ya Chato ililenga kulima jumla ya Hekta
71,267 za mazao ya chakula ambapo tulitarajia kuzalisha tani 298,696 na hivyo kuwa na ziada ya tani 174,658. Jumla ya Hekta 36,577 za mazao ya chakula zililimwa, sawa na 51% ya malengo, ambapo mavuno yote ni Tani 53,019 (wanga 47,962 na protini 5,057) sawa na asilimia 18% ya malengo. Baada ya kutoa maganda/makapi, chakula halisi ni tani 32,978 (wanga tani 27,921 na protini tani 5,057).
Wilaya ya Chato inakadiriwa kuwa na watu 420,191 (kwa mujibu wa taarifa ya NBS mwaka 2017), na mahitaji yake ya chakula kwa mwaka 2017/2018 ni tani 88,071 za wanga na tani 35,967 za protini.
MALENGO YA KILIMO NA UTEKELEZAJI MSIMU WA 2017/2018
Katika msimu huu wa kilimo Wilaya imelenga kuzalisha jumla ya Tani 245,520 za mazao ya chakula sawa na kulima hekta 65,194.4 uhamasishaji unaendelea. Kwa Upande wa mazao ya Biashara malengo ni kuzalisha tani 16,904 sawa na kulima hekta 14,195.2.
Eneo linalofaa kwa kilimo cha Umwagiliaji ambalo ni hekta 10,810 na kuanza uendelezaji wake ambapo hadi sasa hekta zinazomwagiliwa kwa njia mbalimbali ni 3416 sawa na asilimia 31.6% ya eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.
Mkakati mkubwa wa Wilaya kwa sasa ni ujenzi wa skimu kubwa na ndogo ili kuongeza eneo linalomwagiliwa ambapo kwa sasa ujenzi wa skimu ya umwagiliaji katika kijiji cha Nyisanzi kupitia Mpango wa kilimo wa Wilaya (DADP) kwa thamani ya Tshs. 881,557,416.40 umesimama kutokana na uhaba wa fedha ambayo ikikamilika itaweza kumwagilia hekta 250 na kuongeza eneo la umwagiliaji hadi kufikia hekta 3666. Mradi huu unatekelezwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji lakini hata hivyo ni kwa muda mrefu sasa Mradi huu umesimama licha ya juhudi za uongozi wa Wilaya kufuatilia Wizarani.
Aidha tumetekeleza Mradi mmoja katika kijiji cha Kibehe, kitongoji cha Masasi Kwa kuchimba kisima kirefu Kwa ufadhili wa shirika la Tumaini Fund. Kwa sasa Shirika la Tumaini Fund limeanza upanuzi wa mradi wa kutoa maji ziwa Victoria kwa umbali wa kilomita 4 ambao utakua na uwezo wa kumwagilia Hekta 75 sawa na Ekari 187.5
Katika juhudi za kuendeleza kilimo cha umwagiliaji Wilaya ya Chato, timu ya umwagiliaji wilaya kushirikiana na Timu ya kanda (Zonal Irrigation Office) tulifanya utambuzi (Reconnaissances) wa maeneo/mabonde muhimu (Nyamirembe-Masasi, Kibumba, na Makurugusi) kwa ajili ya kuendelezwa kwa ajili ya miradi ya umwagiliaji ilifanyika na mapendekezo ya Timu hiyo yalihitaji Wilaya (Kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji) kutafta fedha kiasi cha tsh.500 millioni kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu.
UJENZI WA MRADI WA UMWAGILIAJI KATIKA KIJIJI CHA NYISANZI
Mradi huu unajengwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ukifadhiliwa na mradi wa DASIP na mfuko wa maendeleo ya umwagiliaji wilayani (DIDF). Mkataba wa mradi huu ulisainiwa na ofisi ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika tarehe 24/05/2013 baina ya wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Mkandarasi kampuni ya NYAKILANG’ANI CONSTRUCTION LTD ya Musoma kwa kutekelezwa ndani ya siku 270 akisimamiwa na mhandisi mshauri ambaye ni kampuni ya CODA Consulting company and Partners ya nchini Kenya kwa thamani ya Tshs. 881,557,416.40. Utekelezaji wa mradi huu ulianza kwa kusuasua na mkataba wake umemalizika tangu 06/02/2014.
Mpaka sasa utekelezaji wa mradi huu bado haujakamilika, utekelezaji umesimama na wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi haijatoa mwongozo wowote licha ya kuandikia barua tatu kwa wakati tofauti.
Mradi huu ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia hekta 250 za kilimo cha umwagiliaji ambapo zaidi ya wakulima 150 watanufaika.
Hali Halisi ya Ujenzi wa Mradi Hadi Sasa
Hadi sasa kazi iliyofanyika ni ujenzi wa tuta refu lenye urefu wa mita 470 yaani Earth embarkment na sehemu ya kutoroshea maji (spillway) ndio zimejengwa hata hivyo spillway haijajengewa na mawe ili kukazia isije ikageuka kuwa korongo. Aidha miundombinu mingine haijajengwa kama ilivyopangwa kwenye usanifu (design). Miundombinu hiyo ni ujenzi wa mitaro mikuu na midogo sambamba na vigawa maji/mabanio (Diversion boxes), kuweka mipaka na vitoa maji Bwawani (outlets), Upandaji wa nyasi downstream kwenye tuta hii ni pamoja na upangaji wa mawe upande wa juu wa tuta (upstream) na kufanya backfill ya borrowpit za vifusi.
CHANGAMOTO KATIKA SEKTA YA KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA
HATUA ZINAZOCHUKULIWA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.