IJUE LESENI YA BIASHARA
Leseni ya biashara ni kibali ambacho hutolewa na mamlaka husika kwa mfanyabiashara au mtoa huduma.
Leseni za biashara hutolewa na wakala wa usajili wa biashara na leseni (brela), halmashauri za manispaa, halmashauri za majiji, halmashauri za miji na halmashauri za wilaya kwa kuzingatia kundi la leseni inayotolewa.
Leseni za biashara zimegawanyika katika makundi mawili A na B.
katika kundi A kuna biashara ambazo leseni zake hutolewa na wakala wa biashara na leseni (brela).kundi hili ni leseni zenye mtaji mkubwa zinazojumuisha leseni za uuzaji wa bidhaa nje ya nchi, huduma za mawasiliano, bandari, vilabu vya usiku, sonara, uchimbaji madini, uuzaji na usambazaji silaha, vyombo vya habari, hoteli za kitalii, huduma za kifedha, taasis za kifedha na mitaji,bima n.k
katika kundi B ni leseni zinazotolewa na halmashauri za manispaa, halmashauri za majiji, halmashauri za miji na halmashauri za wilaya. Katika kundi A kuna biashara za viwanda vidogo, hoteli zisizo za kitalii, vyama vya ushirika, makumpuni ya ujenzi, taaluma muhimu, zahanati, maduka ya dawa muhimu za binadamu, pembejeo za kilimo, migahawa,kalakana, uandishi wa vitabu na magazeti, vituo vya mafuta, spea mbalimbali, shule za binafsi, minada, pembejeo za kilimo, wahandisi wa umeme, maduka ya kuuza bidhaa kwa jumla na reja reja n.k
Biashara za kundi B leseni zake hutolewa na halmashauri ya eneo husika ambapo biashara inafanyika
Utoaji wa leseni za biashara unazingatia kifungu cha 11(1) cha sheria ya leseni za biashara namba 25 ya mwaka 1972 na marekebisho yake
Gharama za leseni hubadilika mara kwa mara kulingana na inavyopendekezwa na mamlakahusika.
Kufanya biashara bila leseni ni kosa kisheria hivyo ni vyema kuchukua hatua za kurasimisha biashara yako kisheria
Maombi ya leseni ya biashara
Ili kupata leseni ya biashara muombaji:-
Nyaraka zote zinazo hitajika ziambatanishwe pamoja na fomu ya maombi
Kumbuka
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.