Wajumbe wa kamati ya Jumuiya ya Tawala za mikoa (ALAT) Mkoa wa Geita inayoundwa na madiwani 2, Mwenyekiti wa halmashauri pamoja na Mkurugenzi Mtendaji kutoka kila wilaya, wameipongeza halmashauri ya wilaya Chato kwa namna inavyotekeleza miradi ya maendeleo kwa kuzingatia ubora wenye kiwango cha juu.
Pongezi hizo zimetolewa leo April 13, 2024 na wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wake Mhe.Vicent Busega Lubaga ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe akiwa ni diwani wa kata ya Nhomolwa walipotembelea ujenzi wa soko la samaki linalojengwa kijiji cha Chato kata ya Chato pamoja na ujenzi wa zahanati ya kijiji cha mlimani kata ya Muungano wilayani hapa.
Ujenzi wa zahanati ya kijiji cha mlimani umegharimu kiasi cha Tsh.106,000,000/= (milioni mia moja na sita tu) mpaka kukamilika kwa mchanganuo wa 32,000,000/= nguvu za wananchi, 24,000,000/= kutoka kwa wadau wa maendeleo na 50,000,000/= kutoka Serikali kuu, zahanati tayari imekamilika na inatoa huduma kwa wananchi.
Walitembelea pia mradi wa ujenzi wa Soko la Samaki lenye vizimba 24 uliopo kijiji cha Chato kata ya Chato ambao utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.7 (bilioni moja na milioni mia saba tu) fedha kutoka Serikali kuu kupitia wizara ya mifugo na uvuvi na mkandarasi wa mradi ni SHIRIJI CONSTRUCTION LTD huku hatua za ujenzi zikiwa ni 83% na mradi unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi june 2024.
Katika ujenzi wa Soko la Samaki pia kutakuwa na ujenzi wa jengo la kuhifadhia samaki wabichi (Cold room), jengo la kuzalisha barafu (ice room), jengo la utawala, jengo la chanja za umeme za kukaushia dagaa, chanja za nje, jengo la mama lishe lenye vyumba 6, jengo la mlinzi pamoja na jengo la matundu ya vyoo vya ME na KE.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Chato Mhe. Batholomeo Manunga ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa namna inavyoendelea kuboresha miundo mbinu kila sekta hususani katika wilaya ya Chato ambapo amekiri kuwa wananchi wa Chato wamefarijika na kufurahi mno kwa uwepo wa Soko hili na wanatamani ujenzi ukamilike mapema ili waanze kunufaika kwa kukuza uchumi wa kaya, wilaya na Taif
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.