Mhe Mkuu wa wilaya ya Chato Bi. Martha Mkupasi amewaambia washiriki wa Kongamano la Kusheherekea Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Uhuru lililofanyika 9 Disemba 2022 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Jikomboe kuwa maendelo ya Chato kabla na baada ya kuundwa rasmi yanakwenda kwa kasi ya hali ya juu.
Jambo ambalo sisi kama watanzania wengine nchi tunapoadhimisha Sherehe hiz I za Uhuru hatuna budi kujipongeza lakini pia kumshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo sisi kama wanachato amekuwa akituletea fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo, amesema ‘kwa mfano katika kipindi cha mwaka huu wa fedha sisi kama wilaya tumepokea zaidi ya bilioni 40 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo’
Fedha hizo zimekwenda katika kutekeleza miradi ya Elimu, Maji, Afya na katika Mindombinu ya Barabara ambapo mpaka sasa kwa mwaka huu wa fedha tulikuwa na ujenzi wa madarasa 185 amabyo yanagharimu Zaidi ya biliono 3.7 ambayo yamekwisha kukamilika kwa zaidi ya asilimia 90 na yanasubiria kupokea wanafunzi wapya wa Kidato cha Kwanza mapema mwakani 2023
Lakini pia ndugu zangu wanachato sisi kama watanzania wengine tunamengi ya kujivunia na kujipongeza kwani upekee sana wilaya yetu imebarikiwa kuwa na miradi mikubwa ambayo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa jambo ambalo hata maeneo mengine kama uwepo wa Uwanja wa Ndege wenye hadhi ya Kimataifa, Hospitali ya Rufaa ya Kanda, Chuo cha VETA na Barabara za Lami katika mitaa yetu.
Nae Katibu Tawala wilaya Ndg. amewashukuru wananchi wote kwa kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya sherehe za Uhuru mwaka 2022 ambazo kwa mwaka huu tumesheherekea kwa kushiriki katika shughuli za kijamii ambazo ni Upandaji wa Miti katika shule ya Msingi Katemi iliyopo kijiji cha Mlimani kata ya Chato, Usafi wa Mazingira katika Soko la Jioni kijiji cha Mkuyuni Kata ya Muungano, Bonanza la Michezo katika viwanja vya Hayati Magufuli na leo tunahitimisha hapa katika viwanja vya Shule ya Sekondari Jikomboe kwa Mdahalo tukifafakari wapi tumetoka na nini kimefanyika ndani ya miaka 61 ya Uhuru.
Akitoa mada Kuhusu Historian a mafanikio tuliyopata tangu tupate Uhuru Mzee Samwel Bigambo ambaye ni mkazi wa Chato amewaasa vijana kuwa mafanikio yote haya tunayoyaona kama hatuta Linda na kutunza Amani ya Nchi yetu basi mafanikio haya tunayojivunia itakuwa ni kazi bure kwani Maendeleo na Amani vinakwenda sambamba kimoja kikikosekana basi kingine hakiwezi kupatikana.
Akihitimisha Kongamano hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chato Bw. Mandia Kihiyo amewataka wananchi kila mmoja kuwa mlinzi wa miradi ambayo inatekelzwa pamoja na rasilimali zilizopo kwani uharibifu unapotokea basi kama wilaya tunakuwa tumerudi nyuma.
Pia Mandia amewakumbusha vijana falsafa ya uwajibikaji na kujitegemea ili kujiletea maendelo yao wenyewe kama ambavyo Mama Mhe Dkt. Samia amekuwa akisema kila mmoja afanye kazi chini ya kauli mbiu ‘Kazi Iendelee’
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.