Maadhimisho hayo yamefanyika katika Kata ya Bwanga katika Kijiji cha Bwanga ambapo viongozi, watumishi wa umma toka taasisi mbalimbali pamoja na wananchi katika maeneo hayo wameshiriki kufanya usafi.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na wakazi wa maeneo ya Bwanga Bi. Fransisca Charles ambaye ni Afisa Afya wilaya amesisitiza wananchi kulinda na kutunza Usafi wa Mazingira kuzunguka maeneo yao ya makazi na biashara kwani kwa kufanya hivyo sote kwa pamoja tutakuwa tumejikinga dhidi ya magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Chato Ndg. Geraid Mgoba pamoja na kusisitiza wananchi kujenga tamaduni za kutunza Usafi wa Mazingira yao, huku akiiwakumbisha kuwa kama wilaya tunatarajia kupokea Mwenge wa Uhuru 30 Septemba, 2024 hivyo basi, Usafi ukawe ni jambo Endelevu"
Pia amewataka wananchi wa maeneo ya Bwanga na viunga vyake kuchanagamkia fursa ya kuchukua vibanda katika Standi mpya ya Bwanga kwani kwa kufanya hivyo tutakuza uchumi na ustawi wa maisha yetu ya kila siku, kuliko kusubiri watu kutoka nje ya maeneo yetu.
Akihitimisha Maadhimisho hayo Mhe. Mkuu wa wilaya ya Chato Ndg. Lous P. Bura ambaye aliwakilishwa na Ndg. Alexander Msisiri amewashukuru wananchi wa Kata ya Bwanga pamoja na vitomgoji vyake kwa namna ambavyo wamejitokeza katika kufanya usafi wa Mazingira kwani kitendo hicho tu ni ishara ya uzalendo kwa nchi kwa Taifa letu kwa ujumla.
Aidha amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kwani uchaguzi huo ndo Msingi wa chaguzi za Viongozi katika Serikali na maeneo yetu ya Utawala toka ngazi ya kitongoji na Kijiji.
Mwisho amewataka wananchi kijitokeza kwa wingi katika uboreshaji wa daftari la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa litakaloanza kuanzia tarehe 11 hadi 20 Oktoba, 2024 kwani bila kufanya, hutaweza kuchagua kiongozi, kwani Kitambulisho cha Mpiga kura hakitatumika mpaka Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais 2025
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.