Halmashauri ya Wilaya ya Chato ikiungana na Taasisi Binafsi na za Umma, wakazi wa eneo husika na wadau wengine wameungana na maeneo mengine duniani kuadhimisha siku ya Usafishaji Duniani ambayo hufanyika Sept 20 kila mwaka, kwa kufanya usafi wa kufagia,kuzibua mitaro iliyoziba pamoja na kukwetua nyasi ikiwa ni katika harakati za kutunza mazingira lakini pia kuboresha afya.
Maadhimisho hayo kiwilaya yamefanyika kijiji cha Mkombozi, Kata ya Muganza leo Septemba 20, 2025, yakiongozwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Fransisca Charles ambaye ndiye Afisa afya wa Wilaya, amesema usafi una umuhimu mkubwa katika maisha ya kila siku, usafi ni afya na ukitunza mazingira yatàkutunza kwa kukuepusha na maradhi, utakuwa na afya njema, ametoa wito kwa kila mmoja kufanya usafi ni wajibu wake na zoezi endelevu katika maeneo yanayomzunguka ili kuipa afya yake kipaumbele.
Bi. Fransisca amewapongeza walioshiriki kikamilifu zoezi hilo muhimu, hususani TARURA,CHAWASA, RUWASA,BENKI YA POSTA,Jeshi la Polisi na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kwa ushirikiano mkubwa,watumishi wote walioshiriki pamoja na wananchi wa eneo husika, ametoa angalizo a yeyote atakayebainika anatupa taka hovyo hususani kwenye vyanzo vya maji amesema sheria zipo zitatumika dhidi yake kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wa maji ambayo tunayatumia sisi wenyewe,madhara yake ni kupata magonjwa ya milipuko hivyo kila mmoja anatakiwa kuwa mlinzi wa mwenzie
"Hongereni sana kwa kazi nzuri yenye maslahi mapana kwa afya zetu,niwapongeze wote mlioshiriki kikamilifu, Taasisi zote mliofika hakika mmewakilisha vema Taasisi zenu,watumishi wote pamoja na wenyeji wetu katika eneo hili hakika kazi imeonekana,tuhakikishe zoezi la usafi linakuwa endelevu, mazingira yakiwa safi na afya zitakuwa safi.Ndg.Zangu leo Mgeni wetu rasmi alipaswa kuwa Mhe.Mkuu wa Wilaya yetu na alitamani sana kuja kuonana nanyi, lakini kutokana na dharula iliyo nje ya uwezo ameshindwa kufika lakini anatambua mchango wenu mkubwa katika kufanikisha zoezi hili muhimu anawapongeza sana" Alisema Bi. Fransisca
KAULI MBIU: “Tunza Mazingira kwa Kuzipa Taka thamani”
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.