Ziara ya Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe. Said J. Nkumba Mnamo Mei 21, 2024 imetembelea na kukagua ujenzi wa Chuo Cha IFM kinachojengwa wilayani humo na kinatarajiwa kukamilika mnamo mwezi June 2024.
Akisoma taarifa ya mradi Mkurugenzi wa Kampasi hiyo Ndg Michael Bukwimba amesema kuwa ujenzi huo utagharimu kiasi cha Tshs.. 8,453,814,447.00 mpaka kukamilika kwake huku akitaja chanzo cha fedha hizo kuwa ni ruzuku kutoka Serikalini pamoja na mapato ya ndani ya Chuo hicho.
Aidha Bukwimba ametaja miundo mbinu inayojengwa kuwa ni jengo la madarasa (wanafunzi 320), utawala (watumishi 46), jengo la mihadhara (watu 500), Maktaba na Tehama (watu 240), Jengo la chakula (watu 200), Mabweni ya wanafunzi 4@112= watu 448, Nyumba za wafanyakazi za familia 8, viwanja vya michezo, miundombinu ya maji na umeme pamoja na barabara.
Mhe. Nkumba amefurahishwa na ubora/uimara wa majengo ya Chuo hicho pamoja na ukubwa wake wakumudu kuchukua wanafunzi wengi kwa wakati mmoja hivyo ameshauri kianze kutangazwa mapema ili utakapo fika muda wa udahili kazi iwe nyepesi
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.