Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato, ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji (W) Ndg Mandia Kihiyo, imeipongeza timu ya mpira wa miguu ya watumishi wa Wilaya hiyo kwa kuibuka kidedea wa Soka katika Bonanza la watumishi wa Mkoa wa Geita lililoandaliwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Martine Shigela na kufanyika Julai 26, 2025.
Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 28, 2025 mara baada ya Afisa utamaduni na Michezo(W) Ndg .Halfan Mbonde (wa kwanza kushoto) aliyeambatana na Nahodha wa timu hiyo Ndg Berino Msigwa kitaaluma ni Afisa Kilimo (wapili kutoka kushoto) walipomkabidhi Mkurugenzi Mtendaji Kombe walilolitwaa katika Bonanza hilo wakati Timu hiyo ya Menejimenti ikiwa katika kikao cha kujadili utendaji kazi wa Halmashauri katika ukumbi wa mikutano wa Wilaya hiyo.
Bonanza hilo lilifanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Wasichana Nyankumbu iliyopo mkoani humo ambapo michezo mbalimbali ilichezwa ukiwemo Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, kukimbiza yai kwenye kijiko, kucheza bao, kukimbiza kuku pamoja na mingine mingi ya kuimarisha viungo.
Mbonde Ameeleza kuwa watumishi wa Chato walishiriki michezo ya Mpira wa Miguu, kukimbiza kuku, kukimbia na yai kwenye kijiko, Mashindano ya kula pamoja na mchezo wa bao huku ikipata ushindi katika Soka kumpata golikipa bora ambaye ni Mwl Karim Hamis wa S/Msingi Nyambiti kata ya Nyamirembe na mfungaji bora Mwl Jabiri Mgovano wa S/Msingi Izenge kata ya Buseresere, wakati kwa upande wa mkimbiza kuku akiibuka mwamba Ndg Frank Ipugute (Afisa Mifugo) na kukimbia na yai akiibuka mshindi wa 3 Ndg Martine Babere mtendaji wa kijiji cha Songambele - Iparamasa.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji Ndg Kihiyo amewapongeza waandaji wa Bonanza lakini pia washiriki wote hususani kutoka Chato kuanzia viongozi wa timu wakiongozwa na Nahodha Ndg Msigwa, wachezaji wa michezo yote pamoja na washangiliaji kwa kufanikisha kombe kuja Chato ni heshima kubwa na wameiwakilisha vema wilaya, huku akiwataka kujiimarisha zaidi kwa mazoezi kwani wakumbuke Bonanza hilo la watumishi Mkoa wa Geita lilikuwa na lengo la maandalizi ya michuano ya Shimishumita kitaifa yatakayofanyika mwezi Agosti 2025 Jijini Tanga.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.