Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya wilaya ya Chato ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndg Mandia Kihiyo, jana Mei 26, 2025 ilitembelea na kukagua miradi ya Maendeleo yenye thamani ya Tsh. 1,977,018,839.29 inayotekelezwa kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo fedha kutoka mapato ya ndani, Serikali kuu pamoja na wahisani.
Miradi ilotembelewa na kukaguliwa ni ujenzi wa taa za barabarani (500,000,000/= kata ya Buseresere), mabweni 2, nyumba ya watumishi 2 in 1 na vyoo matundu 10 (381,000,000/= Kabantange Sekondari), jengo la X - ray kituo cha afya Bwanga (54,000,000/=), OPD Zahanati ya Nyakayondwa (92,410,714.29), ukamilishaji zahanati ya kijiji Minkoto (15,000,000/=), ukamilishaji vyumba 2 vya madarasa s/msingi Nyarubele (10,000,000/=), ukamilishaji zahanatj ya Imwelo (3,000,000/=) Shule mpya shikizi ya Sekondari Mwendakulima Butengorumasa (584,280,029/=), Bweni la wanafunzi Mkungo Sekondari (138,264,048/=), Bweni la wanafunzi Sekondari Butengorumasa (138, 264,048/=), ukamilishaji nyumba ya waganga 2 in 1 zahanati ya kijiji Butengo (50,000,000/=) pamoja na ukamilishaji vyumba 2 vya madarasa s/msingi Maendeleo (10,800,000/=)
Ziara hiyo ya wataalamu yenye lengo la kufuatilia na kuhakikisha utekelezaji wa miradi unafanyika kitaalamu ili kupata miradi yenye ubora wa kiwango kizuri na inayoendana na thamani ya fedha, ilibaini asilimia kubwa ya miradi ipo hatua ya ukamilishwaji lakini pia kwa ile michache yenye changamoto timu ilitoa maelekezo ya kuongeza kasi ya kazi kwa kuongeza mafundi ili kukamilika kwa wakati iweze kuwanufaisha wananchi ikiwa ni kutimiza lengo la Serikali.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.