Mkuu wa Wilaya ya Chato,mheshimiwa Louis Bura amewakabidhi pikipiki maafisa mifugo wa wilaya, ikiwa ni juhudi za serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuimarisha huduma za mifugo ikiwemo chanjo na uogeshaji. Akiwakabidhi pikipiki hizo Mhe.Bura amewasihi maafisa mifugo kuzitunza vizuri pikipiki hizo kwa kuzifanyia service kwa wakati ili zidumu kwa mda mrefu na kusaidia kukuza mapto ya sekta ya Mifugo.
“Ndugu maafisa nyinyi ni mashahidi wa jitihada za serikali katika kutoa huduma bora kwa Wananchi.Sekta ya mifugo sasa ina mabadiliko makubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma hakukua na nyenzo za kufanyia kazi, Serikali imefanya jitihada kuleta nyenzo hizi kwahiyo tunategemea muwahudumie wananchi kwa bidii ili tuapate mapato mengi. Ukipewa kingi,Utadaiwa Kingi” Bura.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Geriad Mgoba amesema kwa kipindi cha mwaka mmoja 2024/2025 Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendelea kuimarisha huduma za mifugo ambapo mpaka mwezi juni jumla ya Lita 216 zimeletwa kwaajili ya Uogeahaji. Pia katika kuboresha huduma za Ugani Wizara imetoa pikipiki 14 kwa awamu mbili mwaka huu.Pikipiki 6 awamu ya kwanza na pikipiki 8 awamu hii ya pili ambazo zitatumika kwaajili ya huduma za Ugani.
Akishukuru kwa niaba ya maafisa mifugo waliokabidhiwa pikipiki hizo, Bi. Arafa Mringo Afisa Mifugo Kata ya Muungano, ameishukuru sana Serikali kwa kuwapatia Usafiri huu utakaowawezesha kuwafikia wafugaji wengi. “Pikipiki hizi zitatuwezesha kutoa huduma ya chanjo kwa Uafanisi, urahisi na kwa muda mfupi”.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.