Mkulima Hodari wa zao la pamba msimu wa 2023-2024 Walwa Malimi, amekabidhiwa trekta jipya na Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe.Louis Bura lililotolewa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kama chachu kwake kuboresha na kuzalisha pamba kwa wingi msimu mpya wa 2024-2025.
Akiongea na hadhara ya wageni waalikwa katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye viunga vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Mhe. Bura amempongeza Ndugu Walwa kwa kuibuka mkulima hodari Nchini,Mheshimiwa amewapongeza maafisa Ugani kwa kutembelea wakulima na kuwafundisha kanuni bora za kilimo cha pamba. Aidha ameagiza kuundwa kwa kamati maalumu itakayohusisha Mkulima hodari,mkuu wa wilaya,baraza la madiwani,maafisa Ugani na kusimamiwa na Afisa Kilimo wilaya ili kuzunguka vijijini kuhamasisha na kutoa elimu ya zao la pamba.
Akitoa ushuhuda namna gani amefanikiwa kuibuka mkulima hodari,Ndugu Walwa Malimi amesema alizingatia masharti ya kipimo cha 60 kwa 30, kukatia vitumba na kuzingatia elimu aliyokua akipewa na Afisa Kilimo wa Kata aliyekua akimzungukia mara kwa mara. Aidha Walwa amewasihi wakulima wenzie kufata masharti ya vipimo ili kuzalisha pamba nyingi na kujikwamua na umaskini.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.