Kamati ya Mfuko wa Jimbo katika Halmashauri ya wilaya ya Chato, ikiongozwa na Mhe. Mbunge wa Jimbo la Chato Dkt. Medard Kalemani mapema hii leo Januari, 7 2025 imefanya ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa jimboni humo ikiwa ni utaratibu wake iliyojiwekea kutembelea Miradi iliyoipa fedha ili kuona matumizi ya fedha hizo na ubora wa Miradi hiyo.
Itakumbukwa kuwa Serikali kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka utaratibu wa kutoa fedha katika Majimbo ya Uchaguzi kwa ajili ya kuchochea Maendeleo ambapo katika Halmashauri ya Chato jumla ya kiasi cha shilingi Milioni 92 kimepokelewa kwa ajili ya kuchochea Maendeleo jimboni humo.
Akiongea na wananchi wa Chato katika maeneo mbalimbali ambapo kamati hiyo imepata fursa ya kutembelea Miradi hiyo ya Maendeleo Mhe. Dkt Kalemani amewapongeza viongozi wa Chama na Serikali kwa namna ambavyo wanashirikiana kitu ambacho kimeleta tija na ubora katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Aisha Mhe. Kalemani amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa namna ambavyo Chato ameendelea kuipatia fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, ambapo kwa Mwaka huu Chato imepokea zaidi ya Bilioni 192 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali mfano Ujenzi wa Maktaba ya Kisasa, Barabara, Miradi ya maji, Shule za Kidato cha Tano na Sita, vyumba vya Madarasa pamoja na upanuzi wa Huduma Afya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Ndg. Mandia H. Kihiyo aliye wakilishwa na Afisa Mipango Bi. Christina Mhina ameihakikishia kamati hiyo akisema, "sisi kama watendaji tunawahaidi kuendelea kusimamia Miradi ya Maendeleo kwa kuzingatia viwango na ubora unaotakiwa"
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.