Serikali mkoani Geita imeziagiza Halmashauri zote mkoani humo kutenga fedha kwa ajili ya upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hizo.
Agizo hilo limetolewa leo na Katibu Tawala Wilaya Chato Bwana Elias Makory kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita kwenye maadhimisho ya siku ya kitaifa ya upandaji miti ambayo kimkoa yamefanyika Wilayani Chato kata ya Bwanga na kwenda sambamba na zoezi la upandaji wa miti katika eneo la ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Nyarututu.
Bwana Makory amesema kila Wilaya kwa mwaka inatakiwa kupanda angalau miti milioni moja na nusu ambapo amesititiza Halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya zoezi hilo.
Katika hatua nyingine Bwana Makory amewaonya wananchi wanaovamia hifadhi za misitu na kufanya shughuli za kilimo, ufugaji pamoja na uchimbaji wa madini ndani ya hifadhi bila kibali cha wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kwani wamekuwa wakiharibu mazingira ya hifadhi hizo na kukwamisha jitihada zinazofanywa na TFS za upandaji wa miti.
Meneja wa wa shamba la Miti la Bihalamulo Bwana Thadeo Shilima amesema kutokana na uharibifu mkubwa wa shughuli za kibinadamu katika hifadhi ya msitu wa Biharamulo Kahama hususan katika eneo la Chato serikali iliamua kuanzisha rasmi shamba hili mwaka 2017/2018 ambalo ni la pili kwa ukubwa Tanzania likiwa na ukubwa wa hekta 69,758 baada ya lile la Sao Hill lililopo mkoani Iringa.
Amesema tangu kuanzishwa kwa shamba hilo hadi sasa wameshapanda miti kwenye eneo la ukubwa wa hekta 522 sawa na miti 579,942 sawa na asilimia moja ya eneo lote la shamba.
Bwana Shilima amesema baada ya miti kukua wanatarajia malighafi zitakazopatikana zitatumika katika viwanda vya kuzalisha karatasi na nguzo za umeme ambapo na tangu kunzishwa kwake jumla ya ajira za muda 600 zimeshatolewa kwa wananchi wanaozunguka shamba hilo pamoja na uanzishaji wa bustani yenye miche zaidi ya 900,000.
Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni “Tanzania ya Viwanda inawezekana, panda miti kwa maendeleo ya Viwanda”.
Meneja wa shamba la miti la Biharamulo Bwana Thadeo Shilima (aliyeshika simu mkononi) akifafanua jambokuhusu aina ya miti kwa mgeni rasmi na wageni wengine wengine walio tembelea shambani hapo
Katibu Tawala Wilaya ya Chato Bwana Elias Makory akipanda mti kwenye eneo la ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nyarututu
Katibu wa CCM Mkoa wa Geita Bwana Clemence Mkondya akipanda mti kwenye eneo la ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nyarututu
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.