Lengo la Kikao: Kikao hicho kilifanyika ili kuimarisha mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa Marburg na magonjwa mengine ya mlipuko, pamoja na kutoa elimu kwa jamii kuhusu hatua za kujikinga.
Washiriki: Kikao kilihusisha viongozi wa serikali, wataalamu wa afya, na wajumbe kutoka jamii mbalimbali, pamoja na wadau wa afya kutoka ndani ya wilaya
Elimu na Ufahamu: Katika kikao, washiriki walipatiwa mafunzo kuhusu dalili za ugonjwa wa Marburg, njia za maambukizi, na hatua za kukabiliana na ugonjwa huo. Mambo kama usafi binafsi, ufuatiliaji wa afya, na umuhimu wa kupata matibabu ya haraka kwa magonjwa nyemelezi kama Homa Kali, Kutapika na mengineyo.
Mikakati ya Kuzuia: Walijadili mikakati mbalimbali ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Marburg, ikiwa ni pamoja na uhamasishaji wa jamii, kuimarisha mifumo ya afya, na ufuatiliaji wa wagonjwa kwa ukaribu zaidi, ikiwa ni sambamba na kuhakikisha jamii inaweka vitakasa mikono mda wote katika makazi na katika sehemu za taasisi za umma.
Ushirikiano wa Kisayansi: Kikao hiki pia kilihusisha mipango ya kushirikiana na taasisi za kitaifa katika tafiti za kiafya kuhusu magonjwa ya mlipuko, ili kuboresha ufanisi katika kukabiliana na changamoto hizo.
Mafunzo ya Vitendo: Ili kuhakikisha kwamba maelezo na mikakati iliyoanzishwa yanatekelezwa kwa ufanisi, washiriki walipata mafunzo ya vitendo kuhusu jinsi ya kutoa huduma za afya na jinsi ya kuzingatia protokali za afya.
Tathmini ya Hatari*: lakini pia Kikao kilikuwa na lengo la kufanya kutathmini juu ya hatari inayoweza kutokea ikiwa jitihada za maksudi hazitofanyika ikiwa ni pamoja na kupoteza nguvu kazi katika nchi yetu kutokana na vifo kwani ugonjwa huu hauna tiba.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.