Kamati ya siasa mkoa wa Geita ikiongozwa na Mhe. Mwenyekiti wake Nicholaus Kasindamila, 24 Agosti 2023 ilitembelea Miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Wilaya ya Chato iliyogharimu kiasi Cha Tshs 3,189,792,774.97 na kukiri kufurahishwa nayo, ikiwa ni zoezi la ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) 2020/2025.
Miradi iliyotembelewa na gharama zake ni; ujenzi wa sekondari mpya Mkungo 811,295,774.37, shule ya msingi Nyakato 'B' (Chabula)348,500,000/=, mradi wa maji safi Buzirayombo 38,000,000,000/= , Kituo cha afya katende 500,000,000/=, barabara ya Chato Gineri - Bwina km 8 kiwango Cha lami nyepesi 1,447,997,000/= na barabara ya Paradise - mlimani urefu wa 0.7 kiwango Cha lami nyepesi 500,000,000/=
Licha ya Mhe. Kasindamila kufurahishwa na ubora wa miradi waliyotembelea pis alitoa ushauri Kwa wahandisi na wataalam wengine kuwa karibu na miradi Kwa kutoa ushauri pindi inapoanza kuliko kusubiri iharibike kuitia hasara serikali wakati lengo ni kutoa huduma bora Kwa wananchi na kuzingatia thamani ya fedha katika mradi (value for money).
Hata hivyo Afisa Mazingira idara ya maji Chato Bi Jester Salim Eliwed akisoma taarifa ya mradi alisema mradi wa maji safi wa miji 28 - mji wa Chato, utatekelezwa Kwa miezi 32 ambapo ulianza April - 2023 na unategemewa kukamilika Desemba - 2025 na utahudumia wakazi 185,333 kutoka kata 10 na vijiji 29 vya Wilaya ya Chato na Kijiji kimoja kutoka Wilaya ya Biharamulo.
Aidha, Bi Jester Alizitaja kata na vijiji vitakavyonufaika na mradi ni Kata ya Bukome vijiji vya- Nyabilezi, Bukome, Buzirayombo, Katale,Mkungo na Nyakato, Kata ya Nyamirembe ni Kijiji Cha Nyakakarango, kata ya Bwina vijiji vya - Murumba, Bwina, na Mbuye, kata ya Chato vijiji vya Mkuyuni, Chato, Kitela na msilale, Kata ya Muungano vijiji vya Muungano, Itale, Rubambangwe,Mlimani na Kahumo, Kata ya Ilemela vijiji vya- Nyambogo, Ilemela, Kanyama, Nyangomango, Kata ya Katende ni vijiji vya- Chabulongo, Katende, Ng'hwabaluhi na kijiji Cha Nyamigogo kutoka Wilaya ya Biharamulo.
Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe. Mhandisi Deusdedith Katwale alifafanua kuwa barabara ya Chato Gineri - Bwina inajengwa Kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza Km1 ilijengwa 2019/2020 ilikamilika kiwango Cha lami na inatumika, kwasasa ujenzi unaendelea Ili kukamilisha Km zilizopangwa.
Mhe. Katwale aliongeza kuwa, Kwa niaba ya wananchi wa Chato anamshukuru saana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa barabara ya kuelekea katika makumbusho ya Hayati Rais John Pombe Magufuli (Paradise - Mlimani) ambayo inajengwa Kwa urefu wa 0.7 KM kupitia mfuko wa Jimbo kiasi Cha Tshs 500,000,000/= wakati urefu mwingine wa 0.7 utaendelea kutekelezwa Kwa kadri fedha itakapo patikana ikiwa ni kukamilisha urefu wa 1.4 Km.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.