KAMATI YA SIASA WILAYA YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI NA USIMAMIZI WA MIRADI YA MAENDELEO CHATO
Na Mwandishi wetu – Chato
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Chato wameupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Chato kwa kutekeleza na kusimamia vizuri Mradi wa mbalimbali ya Maendeo ikiwa ni pamoja na mradi wa ujenzi vyumba vya Madarasa kwa ubora na kiwango cha hali ya juu.
Akitoa pongezi hizo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Barnabas Nyelembi alipokuwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo kama ambavyo Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025 inavyosema katika nyanja za Elimu na Afya.
Amezitaka Kata zote kuhakikisha zinatekeleza miradi kwa ubora na viwango na ubora, ametoa mfano Mradi huo wa Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa pamoja na thamani zake anatekelezwa kote nchini Tanzania na sisi kama wilaya tumepokea Zaidi ya Bilioni 1.7 fedha ambazo Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametupatia sisi wana Chato jambo ambalo nasi tunatakiwa kuonyesha kweli Mhe Rais pamoja na Serikali yake haikukosea kutupatia fedha hizo kwa kuhakikisha tunatekeleza miradi hii kwa kiwango kila mmoja katika eneo lake.
Sasa itakuwa ni aibu kuona sehemu moja wametekeleza kwa kiwango na wengine wanasua suasua mfano Kata ya Bwanga mradi wa Ujenzi wa Madarasa umetekelezwa kwa kiwango cha hali ya juu sana nahata ukitizama jinsi madarasa yalivyojengwa kweli unaridhika kwani yanavutia sana.
Mhe. Nyelembi amesisitiza kwa kusema kuwa, ‘ifike mahala sasa kila mmoja katika eneo lake anapopata mradi wa utekelezaji basi ahakikishe anasimamia kwa weledi ili sote kwa umoja wetu tuweze kutekeleza kwa kiwango cha hali ya juu kama maelekezo ya Serikali na Chama yanavyotaka’
Wajumbe wa kamati ya Sisa wilaya wamewataka watendaji wa vijiji pamoja kata ambao miradi ya maendeleo katika maeneo bado haijakamilika kukaa pamoja na kujitathmini kwanini miradi katika maeneo yao haijakamilika kwa wakati kama maelekezo ya Serikali yanavyotaka na kuacha tabia ya kubishana na kutupiana mpira bali kila mmoja atimize wajibu wake.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Ndg. Mandia Kihiyo amewataka watendaji wa Kata na vijiji kushirikiana na jamii kikamilifu katika kutekeleza miradi mbalimbali ya Serikali inapokuwa inatekelezwa katika maeneo yao, kwani kwa kufanya hivyo basi jamii itajiona kuwa sehemu ya mradi na hivyo kuwa walinzi na wasimamizi wazuri katika mradi husika.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.