Akitoa mafunzo hayo Bi. Magdalena Dinawi kutoka Wizara ya Afya kitengo cha Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, kwa wajumbe wa kikao hicho wilaya ya Chato mkoani Geita amesisitiza uwajibikaji kwa kila mjumbe wa kamati kwa kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake.
Aidha Bi. Magdalena ameongeza kwa kusema ili tuwe salama basi kwa umoja wetu ni lazima kila mmoja alinde afya yake na ya mwenzake ili tuhakikishe sote tunaishi mahala salama.
Mkuu wa wilaya Mhe. Deusdedith J. Katwale aliyewakilishwa na Katibu Tawala wilaya ya Chato Ndg. Elias Makory katika kikao hicho ameomba viongozi wote kuanzia ngazi ya jamii hamna budi kwenda kushirikiana kila mmoja kwa nafasi yake uwe kiongozi wa Dini, mtoa huduma za tiba asili au tiba mbadala, muuguzi wa Afya kwa umoja wenu narudia tena nendeni mkashirikiane na jamii katika mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko na majanga ya Afya ndani ya wilaya yetu na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wa Mganga Mkuu wa wilaya ya Chato Dr. Eugen amewaomba wajumbe wa kamati hiyo kwenda kua mabalozi wazuri katika jamii juu ya kuchukua tahadhali za kujikinga na magonjwa haya ya mlipuko kwani sisi kama chato hatupo kisiwani kwamba tumejifungia wenyewe bali tunaishi na watu mbalimbali ambao wanatuzunguka toka kila kona ndani na nje ya nchi yetu, hivyo hatuna sababu ya kuhakikisha kila mmoja wetu anachukua tahadhali katika kuhakikisha Chato inakuwa mahala salama pa kuishi bila magonjwa ya mlipuko kama Kipindupindu, Kovid 19 na Maburg ambayo iligundulika huko Kagera mapema mwanzoni mwa mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chato Ndg. Mandia Kihiyo amesisitiza wataalamu wa Afya kuendelea kutoa Elimu juu ya madhala yatokanayo na magonjwa ya mlipuko hasa katika maeneo yote tunayotolea huduma kwa wananchi.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.