Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri siku ya Jumanne Juni 11 2019 ameiongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akikagua miradi hiyo Mkuu wa Wilaya ameseisitiza wataalamu wa ujenzi kusimamia kwa ukaribu shughuli za ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri hususan miradi inayosimamiwa na kamati za ujenzi za vijiji kupitia mfumo wa ‘force account’.
Mkuu wa Wilaya pamoja na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama pia wamesisitiza vifaa vinavyotumika katika majengo ya serikali viwe vya ubora unaokubalika ili majengo ya serikali yaweze kudumu.
Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri akielekeza jambo kuhusiana na ujenzi wa jingo la OPD kwenye kituo cha afya cha Muganza.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya wakikagua majengo ya kituo cha afya cha Muganza ambacho kinajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 400 kutoka Ofisi ya Rais- TAMISEMI.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya wakikagua ujenzi wa madarasa matatu mapya na bawalo la shule ya sekondari Bwina ambayo mwezi Julai 2019 inatarajiwa kupokea wanafunzi wa kidato cha tano.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya wakikagua ujenzi wa kituo cha afya cha Bwina ambao utagharimu shilingi milioni 500 hadi kukamilika kwake.
Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wakikagua ujenzi wa kituo kipya cha mabasi cha Chato kinachojengwa katika kijiji cha Kahumo kata ya Muungano.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama walifika pia katika mradi wa maji wa Imalabupina Ichwankima, mradi unatogemewa kuhudumia vijiji 11 vya kata za Nyamirembe, Ichwankima, Kachwamba na Kasenga
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.