Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe amewaagiza wataalamu wa kilimo Wilayani Chato kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika zoezi ununuzi wa Pamba linaloanza leo ili wakulima wauze Pamba bila ya kuwepo na malalamiko.
Mhandisi Mtigumwe ametoa agizo hilo leo wakati akiongea na wadau wa Pamba wilayani Hapa, kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa wa Halmashauri.
Amesema kwa msimu huu kwenye kilimo cha zao la Pamba kwa nchi nzima ilitarajiwa kuvuna Pamba tani zisizopungua 450,000 lakini kutokana na hali ya hewa kutokuwa nzuri kutaathiri kufikia malengo hayo hivyo amewataka wataalamu hao kujikitika kwenye msimu ujao kwa kuanza maandalizi mapema Zaidi.
“kwa hiyo tunaweza tusivune pamba kama iliyotarajiwa…, tuanze maandalizi mapema ya msimu ujao, tukiongeza tija kama tunavyotarajia, mkulima mmoja avune pamba kilo 900 kwenye ekari moja tutafikia malengo yetu kwa msimu ujao, tija ndiyo jambo mhimu na hili nalisisiza” alisema Mhandisi Mtigumwe.
Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri amewataka Maafisa Ugani katika kipindi hiki cha ununuzi wa Pamba kuhakikisha wanakuwepo kwenye vituo hivyo na watoe taarifa za kila siku kuhusu ununuzi wa Pamba sambamba na taarifa za wakulima ambao hawajalipwa fedha za Pamba kwa wakati.
Wataalamu wa kilimo wamesema zao la Pamba limekua likiathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na changamoto kadhaa ikiwemo wakulima kutokuzingatia ushauri wa walaalmu kwenye matumizi ya viuadudu na njia bora za kilimo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtugumwe akiongea na wadau wa Pamba (hawapo pichani) kwenye kikao cha siku moja kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri kwa ajili ya kujadili changamoto kuelekea kwenye msimu wa ununuzi wa zao Pamba mwaka 2019 na maandalizi ya Msimu ujao wa kilimo
Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri akiongea na wadau wa Pamba
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo (hayupo pichani)
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.