Wanajeshi kutoka Afrika Kusini wamesheherekea Siku hiyo ya Kuzaliwa Nelson Mandela kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya kujifunza na kujifunzia.
Vifaa vilivyotolewa ni Boxi za Karatasi, Matanki ya Maji, Viti vya plastic, Vitanda vya Chuma, Magodoro, Mabranketi, Mashuka, Mifuko ya Simenti, Ndoo za rangi, na vifaa vingine.
Akiongea Brigedia jenerali Modley kutoka South Africa ambaye ni Mkuu wa kikosi hicho cha wanajeshi kutokea South Africa chini ya mwamvuli ya SIMSADC amesema wao kama Taifa wanasheherekea siku hiyo muhimu ikiwa ni kuyaenzi mambo yote aliyoyafanya mwasisi wa Taifa hilo katika kupigania Uhuru wa nchi hiyo.
Wanajeshi hao wamekuepo wilayani Chato katika kituo chao cha mpito wakitokea wakitokea Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ambapo walikuwa wameambatana na majeshi kutoka nchi za Tanzania, Malawi na Afrika Kusini wakielekea katika nchi zao baada ya kumaliza kazi ya kulinda Amani nchini Congo.
Akizunguza katika Hafla hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chato Ndg. Elimkwasi amewashukuru sana wanajeshi hao kwa kuendelea kudumisha mahusiano mazuri yaliyoasisiwa na watangulizi wao katika kupigania Uhuru wa nchi za Afrika ambao ni Hayati Julius Nyerere pamoja na Nelson Mandela hivyo kitendo kilichofanyika leo katika Shule kimeacha alama kwa vizazi na kwa Vijana hawa wadogo wanaosoma katika Shule hii ambao kimsingi kamwe hawatakuja sahau katika maisha yao yote.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Bi. Salome amewashukuru tena wanajeshi hao kutoka Afrika Kusini huku akiwahakikishia vifaa hivyo vilivyotolewa vitatumika kwa maksudi yaliyokusudiwa tu na si vinginevyo kwani vimekuwa msaada mkubwa sana katika Shule hiyo huku akisema, sisi kama Shule hatuna cha kuwalipa isipokuwa tunawaahidi tutawaombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kuwabariki na kuwapigania katika shughuli zenu za kila siku mtakapo rudi nchini kwenu.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.