Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri (mwenye kofia ngumu ya njano)akipokea maelekezo ya namna ya kutumia pampu ya kunyuzia dawa ya ukoko majumbani kutoka kwa wanyuziaji waliopata mafunzo
Mkuu wa Wilaya ya Chato pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Hlamshauri ya Wilaya ya Chato Eliurd Mwaiteleke (mwenye kofia ngumu nyekundu) wakijiandaa kunyunyuzia nyumba ya mfano kama ishara ya uzinduzi
Mkuu wa Wilaya ya Chato akinyunyuzia dawa ya ukoko kwenye moja ya nyumba ya mkazi wa kitongoji cha Kasenda kama ishara ya uzinduzi wa zoezi la unyuziaji wa dawa ya ukoko mwaka 2018
Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri amesema kila kaya ndani ya Wilaya ya Chato ni lazima ipuliziwe dawa ya ukoko ili kutokomeza ugojwa wa Maralia ambao umekuwa ukiathiri nguvu kazi ya Taifa.
Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo wakati akizindua zoezi la unyunyuziaji wa dawa ya ukoko majumbani kwa Wilaya ya Chato ambalo limefanyika kitongoji cha Kasenda kata ya Muganza.
Mkuu wa Wilaya amesema serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa katika kununua madawa na vifaa tiba kwa ajili ya kutokomeza magonjwa mbalimbali ikiwemo malaria lakini baadhi ya wananchi wamekuwa hawashiriki vyema kwenye vita dhidi ya maralia hususan kupitia mpango wa unyuziaji wa dawa ya ukoko majumbani kwa kutoa visingizio kadhaa.
“Watanzania tunapaswa kuishi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni, zoezi hili la upuliziaji dawa ya ukoko ni la kisheria kwenye afya ya msingi, hivyo nitoe rai kwa wananchi kutimiza wajibu wao na kuwa tayari kunyunyuziwa dawa hizo kwani zimefanyiwa utafiti na ziko salama” alisistiza Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa Wilaya pia amesema kupitia sheria za afya ya msingi ikiwemo ya mwaka 2009 kifungu cha 30 (1-2), ambayo inamtaka kila mwananchi kushiriki katika shughuli za afya za msingi na uvunjaji wa sheria hiyo unaweza kupelekwa mahakani na kuhukimiwa kifungo cha miezi miwili au faini ya shilingi laki moja hivyo amewataka wanachi kuwajibika na kufungua nyumba ili kupuliziwa dawa hiyo.
Jumla ya kaya 119766 zinatarajiwa kufikiwa na zoezi hilo la unyunyuziaji wa dawa ya ukoko majumbani. Maambuki ya maralia kwa Wilaya ya Chato kwa sasa ni ya asilimia 15.5 na lengo la Wilaya ni kuhakikisha inafikia chini ya asilimia 10 ifikapo 2020.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.