Halmashauri ya Wilaya ya Chato imeadhimisha miaka 63 ya Uhuru kwa kufanya usafi na kupanda miti katika stendi ya mabasi Muganza.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mheshimiwa Emmanuel Tagota Diwani wa kata ya Muganza akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya amewashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kufanya usafi kwa umoja na kupanda miti! “Ninaomba kila mtu asimamie mti alioupanda na usafi ufanyike mara kwa mara bila kushurutishwa kwa lengo ya kuzitunza afya zetu”
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Wilaya, Afisa Afya wa Wilaya Ndugu Fransisca Charles amewasihi wananchi kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. “Miti tuliyopanda leo,tuitunze ili itusaidie kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi yanayoathiri shughuli zetu za maendeleo hasa kilimo”
“Tumegawa na kupanda jumla ya miche 215 ya miti ya kivuli, tuna lengo la kuhakikisha Chato inakua ya Kijani” amesema Neema Benson, Afisa Mazingira.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.